Featured Kitaifa

USAMBAZAJI HUDUMA YA MAJI MANISPAA YA IRINGA WAFIKIA ASILIMIA 97

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI  Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Februari 27,2023 jijini Dodoma wakati   kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.

MKURUNGEZI Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo,kuwasilisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo leo Februari 27,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MKURUGENZI  Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo,amesema hadi sasa huduma ya maji safi katika Manispaa ya Iringa imewafikiwa wananchi kwa zaidi ya asilimia 97 na mikakati ya kuwafikia wananchi wote inaendelea.

Hayo ameyasema leo Februari 27,2023 jijini Dodoma wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.

Mhandisi Pallangyo,amesema kuwa IRUWASA imefanikiwa kuhakikisha huduma ya maji Mjini Iringa na maeneo ya pembezoni inapatikana kwa wastani wa saa 23 kwa siku.

“Tunaishukuru sana serikali yetu ya awamu ya sita kwa kutupatia fedha ambapo hivi sasa tunatekeleza miradi ya maji inayogharimu Sh.bilioni 200”amesema  Mhandisi Pallangyo

Aidha amesema kuwa  pamoja na mafanikio hayo mamlaka hiyo bado inakabiliwa na vikwanzo mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira unaosababisha ukame na kupungua kina cha maji.

“Uharibifu wa mazingira ikiwemo uendejai shughuli za kibinadamu umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kukauka kwa vyanzo vya maji na kusababisha utoaji wa huduma kuwa wa mgao”amesema 

Hata hivyo, amesema mamlaka hiyo inaendelea ni jitihada mbalimbali za kuongeza huduma ya uondoshaji maji taka ambapo hivi sasa imewafikia watu kwa asilimia 6.8.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Matumizi ya dira za maji za malipo kabla zimekuwa suluhisho la malalamiko ya wananchi kubabikiziwa ankara na mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini.

”Hadi sasa mamlaka hiyo imefunga dira za malipo ya maji kabla kwa wateja na taasisi mbalimbali zaidi ya 6,700 ambazo zimesaidia kupunguza malalamiko kwa wateja.”ameeleza Mhandisi Pallangyo

About the author

mzalendoeditor