Featured Michezo

YANGA SC ,AS REAL DE BAMAKO WAGAWA POINTI CAF

Written by mzalendoeditor

WAWAKILISHI Katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Timu ya Yanga SC wameshindwa kuondoka na Pointi tatu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji AS Real De Bamako Mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa 26 Mars nchini Mali.

Yanga SC walipata bao la kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari kwa sasa Fiston Mayele dakika ya 60 akimalizia pasi iliyopigwa na Stephane Aziz Ki huku wenyeji wakisawazisha dakika ya 90 likifungwa kwa kichwa na beki Emile Kone.

Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha Pointi 4 nafasi ya pili,US Monastir wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 7,TP Mazembe ikisalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 3 huku As Real De Bamako nafasi ya nne wakiwa na Pointi 2 kundi katika kundi D. 

Mchezo mwingine wa kundi hilo Timu ya TP Mazembe imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa US Monastir katika uwanja wao wa nyumbani mchezo uliochezwa nchini DR Congo.

About the author

mzalendoeditor