Featured Michezo

SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI CAF,YAICHAPA VIPERS SC NCHINI UGANDA

Written by mzalendoeditor

WAWAKILISHI katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Timu ya Simba SC imefufua Matumaini ya kutinga Robo FainaliĀ  baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Vipers SC mchezo uliopigwa uwanja wa St.Marry’s nchini Uganda.

Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wao Henock Inonga dakika ya 20 akimalizia mpira uliopigwa na Moses Phiri.

Huo unakuwa ushindi wa Kwanza kwa Simba baada ya kupoteza mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya Raja Casablanca na Horoya AC.

Kwa matokeo hayo Simba imepanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 3, Raja anaongoza kundi akiwa na Pointi 6 huku Horoya wakiwa na Pointi 4 nafasi ya pili ambazo zitacheza baadae.

About the author

mzalendoeditor