Featured Kitaifa

KAMATI NDOGO JUMUIYA YA WAZAZI DAR ES SALAAM ZINAENDA KUTOA DIRA YA MKOA-BI.KHADIJA SAID

Written by mzalendoeditor

JUMUIYA ya Wazazi  cha cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam wameunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo  ili kuweza kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi ya mkoa huo inakuwa dira ya mkoa na inayokwenda kusimamiwa ndani ya miaka mitano kuweza kuhakikisha inatekeleza 2022/2023 kusimamia mipango kazi ambayo wamejiwekea kwa  miaka  mitano.

Akizungumza katika sherehe za kuwakabidhi barua za uteuzi wanakamati leo Februri 25,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam Bi.Khadija Ally Said amesema anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwenye kamati zilizoundwa katikakuhakikisha kazi za jumuiya ya wazazi ndani ya mkoa wa Dar es salaam wanazitendea haki, 

Kamati ambazo  zimeundwa na kutangazwa ni kamati tano ambazo ni Kamati ya Miradi, Uchumi na Maendeleo, Kamati ya Utamduni, Michezo na Mazingira, Kamati  ya Elimu, Afya na Malezi,Kamati ya Nidhamu na Maadili pamoja na Kamati  ya Habari za Jumuiya.

– Advertisement –

Akizungumza kuhusu Kamati  ya Elimu, Afya na Malezi  Bi.Khadija amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi, malezi  ni  ajenda yeao kitaifa, ndo  maana wanakuja na  kauli  mbiu  ya “Malezi bora kwa Mtoto , Faraja ya Kesho  ya Mzazi na Taifa”, ambapo kamati hii inawataalamu ambao wataenda kufanya mafunzo kwa viongozi wa ngazi  ya kata, pia kamati hii ina viongozi wa kiroho.

“Kamati hii inaenda kusimamia mambo ya msingi sana ya malezi na maadili lakini  pia suala zima la elimu kuhakikisha ufaulu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa watoto wa shule za Msingi na Sekondari unakua, lakini tunaenda kuanzisha shule za awali ambayo kupitia hii kamati wataweza kutuanzishia umuhimu wa shule za awali katika ngazi ya kata, wilaya lakini kuhakikisha kwamba jumuiya ya wazazi  inasimamia elimu  katika ubora wake na afya vilevile”. Amesema

Aidha amesemaKamati ya miradi, Uchumi na Maendeleo inaenda  kusaidia kwa  kiwango kikubwa ndani ya Mkoa kwani katika sera za siasa na uchumi lazima tuwe na miradi ambayo  iko katika  hali sahihi na watafanya kazi katika miradi ambayo Jumuiya ya Wazazi itaweza kubuni, kusimamia na kuiongoza kuhakikisha wanabadilisha hali ya wanajumuiya wake katika ngazi  ya kata,  Wilaya na Mkoa lakini  pia kufanya miradi  ambayo inapeleka jumuiya na chama cha mapinduzi moja kwa moja na wananchi katika  kuongeza kipato chao.

Pamoja na hayo,  miongoni mwa Kamati ambazo  zimeundwa, kuhusu Kamati  ya Utamduni, Michezo na Mazingira, amesema kuwa katika kujenga mahusiano  yetu lazima tuingie kwenye michezo, kwahiyo watakuwa na timu  za wazazi katika kata zao, watakuwa na mashindano  ya michezo mbalimbali katika kata, wilaya na katika ngazi  ya mkoa.

“Tunategemea kama tukifanya vizuri kuingia na kwenda hata nje ya nchi kupitia timu zetu , na hii ni kwaajili ya kupanua wigo wa mahusiano kati  ya Chama lakini  pia na wananchi wake kwahiyo michezo ndio sehemu peke yake watu wanakutana kwa pamoja”.  Amesema   .

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati  ya ya Elimu, Afya na Malezi Bw.Ismail Sadick (Suma lee) amesema atajitahidi  kushirikiana na wajumbe wengine kuhakikisha suala la elimu na malezi linakuwa bora katika  Mkoa wa Dar es Salaam kwasababu katika Kamati hiyo wapo viongozi wa kiimani ambao  pia wataenda kushirikiana nao.

About the author

mzalendoeditor