Featured Kitaifa

RC AYOUB ATAKA WAKULIMA WA KARAFUU KUACHA KUSAFIRISHA KWA NJIA YA MAGENDO

Written by mzalendoeditor

Mku wa Mkoa wa Kaskazin Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Wadau na Wakulima wa Zao la karafuu Wakati alipokua  akifungua Mkutano wa kutathmini zao hilo ulioandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar ZSTC huko Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

Sheikh Swaleh  Ali Mohammed  alipokua  akiwasilisha mada ya  kuzifanyia ghish neema za Allah (israf) wakati wa Mkutano wa wadau  na Wakulima wa Zao la Karafuu ulioandaliwa na  Shirika la Biashara  Zanzibar ZSTC na kufanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

Katibu wa Shirika la Biashara Zanzibar ZSTC  Ali Hilal Vuai (alieshika kinasa sauti) alipokua akitoa tathmini ya utekelezaji wa kazi za Shirika wakati wa mkutano na Wadau na Wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

Wadau na wakulima  wa Zao la  Karafuu  walipokuwa katika Mkutano wa kutathmini zao hilo ulioandaliwa na Shirika la Biashara Zanzibar ZSTC na kufanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

katibu wa Jumuiya  ya Zanzibar cloves producer organization (ZACPO)  Salim sleyum abeid alipokua akitoa salamu za Jumuiya katika mkutano wa wadau na wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

Afisa kutoka Wizara  ya Kilimo Mussa Rajabu alipokua akihamasisha upandaji wa miche ya mikarafuu katika  Mkutano wa kutathmini zao hilo uliowashirikisha Wadau na Wakulima  wa Zao la Karafuu huko Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja

Afisa masoko PBZ Aziza Baraka Omar   alipokua akitoa  elimu ya malipo na kutunza fedha  kupitia Benki wakati wa Mkutano wa wakulima na Wadau wa Zao la Karafuu uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja

Mkuu wa kitengo cha biashara Tigo pesa Haidar Ali  alipokua akitoa elimu kuhusiana na malipo kupitia Ezypesa -Tigopesa wakati wa Mkutano wa Wadau na wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Afisa kutoka  wakala wa vipimo Zanzibar  weight association (ZAWEMA )abdalla Mohammed khamis alipokua akitoa elimu juu vipimo vya uzito na ubora wa karafuuu katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja

Mkulima wa Zao la Karafuu Shehia ya chaani Nyange Omar haji alipokua akichangia mada katika Mkutano wa kutathmini zao hilo uliowashirikisha Wadau na Wakulima wa zao la karafuu huko Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,

Mkuu wa ukaguzi wa Mazao Bandari ya Malindi Hawa Ahmad Iddi alipokua akichangia mada katika Mkutano wa  kutathmini zao hilo uliowashirikisha Wadau na Wakulima wa Zao la Karafuu huko Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, tarehe 25 fubuari 2023.(PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

Na Rahma Khamis- Maelezo  

 

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amewataka wakulima wa karafuu Mkoani humo kuacha kusafirisha karafuu kwa njia ya magendo ili kuzuwia upotevu wa pato la Serekali.

Akifungua mkutano wa wakulima na wadau wa karafuu wa kutahtmini zao hilo katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni amesema kuna baadhi ya watu wanasafisha zao hilo kinyume na sheria jambo ambalo linarejesha nyuma juhudi za Serikali katika kuwainua wakulima.

Amesema zao la karafuu lina historia kubwa kutokana na uchumi wa wananchi kuupata kupitia zao hilo hivyo ipo haja kwa wakulima kulilinda na kulithamini kwa umuhimu wake.

Aidha Mkuu huyo amefahamisha kuwa katika kujitahmini ni lazima kuangalia makosa yaliyojitokeza mwaka jana na kujipanga vyema mwaka huu ili kuweza kuliimarisha zaidi zao hilo

 Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC )Bakari Haji Bakari amesema lengo la mkutano huo ni kupokea changamoto za wakulima wanazozipata wakati wanapokwenda kuuza karafuu katika Shirika hilo na kuzifanyia kazi.

Aidha amewasisitiza wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanazikausha vizuri karafuu zao kabla ya kwenda kuziuza ili kuongeza kipato.

Nao washiriki wa Mkutano huo wameiomba Wizara ya Kilimo kuhakikisha udhibiti wa ugawaji wa miche ili kuwafikia walengwa waliokusudiwa.

Wamesema kuna baadhi ya wakulima wanachukua miche ya mikarafuu na baadae kuiweka vipembeni bila ya kuipanda jambo ambalo sio zuri kwani linawakoseha wengine ambao wanaohitaji zaidi miche hiyo.

Hata hivyo wamelishauri shirika kutoa adhabu kali kwa wale wote wanaoanika karafuu katika sehemu ambayo si salama kwani inapelekea kukosa ubora unaotakiwa.

Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)) kwa kushiriiana na Bank ya Watu wa Zanzibar(PBZ) na Kampuni ya Tigo-Zantel.

About the author

mzalendoeditor