WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Februari 24, 2023 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Kyle Nunas
Lengo la ujio wa Balozi huyo ni kujiatambulisha. Waziri Mkenda ameishukuru Serikali ya CANADA kwa namna inavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwenye Vyuo vya ualimu kupitia Mradi wa TESP na UTC
Katika mazungumzo yao Waziri Mkenda amemweleza Balozi Nunas maboresho ya elimu yanayoendelea nchini ikiwemo kufanya mapitio ya Sera ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mabadiliko ya mitaala, ujenzi wa VETA pamoja na umarishaji wa elimu ya ualimu.
Kwa upande wake Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Kyle Nunas ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua inazochukua katika kuelekea kutoa elimu ujuzi na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliokuwepo baina ya Tanzania na nchi ya Canada.