Featured Michezo

SIMBA SC,AZAM FC ZAGAWANA POINTI,DUBE AFUNGA BAO LA MAPEMA ZAIDI KWENYE LIGI

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Simba SC imeshindwa kutamba mbele ya Azam FC baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Prince Dube amefunga bao la mapema zaidi katika msimu huu baada ya kutumia sekunde 16 kufunga bao la kwanza lililowapeleka Azam mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha Pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko  na katika dakika ya 90 Simba SC walisawazisha bao baada ya beki wa Azam Abdallah Kheri kujifunga kutoka na mpira uliopigwa na Denis Kibu.

Kwa Matokeo hayo Simba SC wanabaki nafasi ya pili wakiwa na Pointi 54 wakiwa wamecheza mechi 23 huku Azam FC wakipanda nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 44 wakilingana na  Singida Big Stars wenye yPointi 44 ,Yanga bado wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 59 wakiwa wamecheza mechi 22.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja KMC watakuwa nyumbani kucheza na Yanga SC 

About the author

mzalendoeditor