Msanii maarufu kutokea nchini Afrika Kusini, Kiernan Jarryd Forbes ‘AKA’ ameripotiwa kufariki dunia kwa kupigwa risasi tano yeye pamoja na mtu mwingine katika eneo maarufu la usiku kwenye Barabara ya Durban ya Florida Ijumaa usiku.
Kwa mujibu wa mhojiwa wa kwanza katika eneo la tukio, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alipigwa risasi akiwa amesimama kwenye lami wakati milio ya risasi ilisikika muda mfupi mida ya saa 22:00.