Featured Kitaifa

PROF.MKENDA :TUMEDHAMIRIA KUKOMESHA VITENDO VYA WIZI WA MITIHANI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2023 jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa Wanafunzi 337 waliofutiwa Mitihani.

……………………

Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imesema imedhamiria kukomesha vitendo vya wizi wa mitihani huku ikiridhishwa na uamuzi wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao ya kidato cha nne mwaka 2022.
 
Hayo yamesemwa leo Februari 8,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia 
Prof.Adolf Mkenda,wakati akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari kufuatia Video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wazazi wa wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari Thaqaafa iliyopo Jijini Mwanza wakiandamana kudai Watoto wao hawajatolewa matokeo ya Kidato Cha Nne.
Prof.Mkenda amesema Wizara hiyo itapeleka marekebisho ya sheria ya baraza hilo bungeni ili hatua zaidi zichukuliwe kwa wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani.
 “Mtihani wa darasa la saba tulivyorudia tulitumia mabilioni ya fedha za watanzania kwa hiyo ni uhujumu uchumi kudanganya kwenye mitihani, polisi wanafanya uchunguzi kwenye hili tunaamini hatua zitachukuliwa na wizara imeridhika na hatua zilizochukuliwa na baraza,”amesema Prof.Mkenda
Amesema kuwaa kati ya watahiniwa 560375 waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022 matokeo ya watahiniwa 337 sawa na asilimia 0.06 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wamefutiwa matokeao kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujaza matusi,kuingia kwenye chumba cha mitihani na maandishi,kuingia na simu na smartwatch.
Prof.Mkenda amesema kuwa serikali imeridhishwa na uamuzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA) kuhusu wanafunzi 337 waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo.
“Sisi uongozi wa baraza tumekutana na kila kundi la wale ambao matokeo yao yamefutwa, tumejiridhisha na tungependa kutoa matokeo yafuatayo wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne ni 560,335 kati ya hao wanafunzi waliofutiwa matokeo ni 337.”
“Hii ni asilimia 0.06 ya watahiniwa wote ni asilimia ndogo sana lakini inagusa watanzania wenzetu wanafunzi wengine 20 matokeo yao hayajafutwa yamezuiwa bado uchunguzi unaendelea na utakapokamilika baraza litachukua hatua stahiki,”amesisitiza
.
 Amesema kuwa Wizi wa Mitihani ni kosa kubwa sana ni sawa na uhujumu uchumi na hatakubaliana nalo na wezi wa mitihani lazima wakamatwe na washughulikie kisheria kwa sababu haivumiliki.
‘Tayari barua zimeandikwa kwa Mamlaka husika juu ya Wasimamizi wa mitihani hiyo kwani Kuna uchunguzi unaonesha Usimamizi ulikuwa Mbovu huku Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi, kwa kuhoji wanafunzi na Walimu ambapo wanafunzi wamekiri.’amesema Prof.Mkenda

About the author

mzalendoeditor