Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi ,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya,,akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Viongozi wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),Dkt. Paul Loisulie,akiapishwa kuwa Kiongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),Dkt. Paul Loisulie,aakisaini nyaraka mara baada ya kuapishwa kuwa Kiongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),wakiapishwa kuwa Viongozi wa Chama hicho hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………
Na. Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto mbambalimba zilizopo katika Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU),ikiwemo kuongeza bajeti ya utafiti na kufanya maboresho ya mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa wana taaluma.
Kauli hiyo imebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa Chama hicho .
Katambi amesema kuwa Serikali kupitia ofisi yake ina jukumu la kutoa na kusimamia sera,sheria,kanuni na miongozo inayowawezesha wafanyakazi kuwa katika mazingira bora ya kazi.
Mhe. Katambi ameeleza kuwa serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na ipo tayari kufanyia kazi changamoto za THTU ili kuwezesha chama kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha kwa kutimiza malengo yake.
“Tafiti zifanyike ili kuhakikisha, Dkt. Samia anatafuta fedha ili kuhakikisha vyuo vinabaki hai na tafiti kufanyika kwa manufaa ya taifa ili kuleta dira ya nchi”, ameeleza Mhe. Katambi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie ameeleza kuwa ushirikiano baina ya THTU na Serikali utasaidia kuwezesha hoja zao kutatuliwa kwa pamoja.
Dkt. Loisulie ametoa wito kwa serikali kutatanisha THTU na wadau wote wanaohusika na masuala ya vyuo vikuu binafsi ili kujadili namna ya kuvisaidia vyuo hivi kutatua changamoto nyingi zinazovikabili.
“Sisi tunaamini kwamba kupitia serikali, kikao cha Pamoja kitawezekana na ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zitajadiliwa na kupatiwa suluhisho”, ameeleza Dkt. Loisulie
Ameendelea kusema kuwa mchango wa tafiti na machapisho katika maendeleo ya nchi wote wanakubaliana juu ya umuhimu wa tafiti katika kutekeleza jitihada za maendeleo kwa nchi.
Katika hilo ameeleza maendeleo yote duniani huletwa kwa utafiti ambao huonesha namna na njia za kupitia katika kufanikisha jambo fulani.
Pia ameongeza kuwa itambulike kwamba utafiti unahitaji uwekezaji mkubwa sana lakini ni gharama isiyoepukika kama dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanatekelezeka kwa ufanisi zaidi.
Vile vile amesema ikumbukwe kwamba, katika wigo wa elimu fedha kutoka nje zinakuja zikiwa na malengo maalum ambayo mara nyingine si lazima yaendane na vipaumbele vya nchi yetu.
Hivyo, ametoa mapendekezo kuwe na mfumo wa kuweza kuzipata taarifa zote za utafiti unao fanyika nchini Tanzania (country research portal/repository).
Pia kuwe na sera na muongozo unao wataka watafiti kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti yanarejeshwa kwenye jamii (walaji/watumiaji) wa matokeo ya utafiti) ili matokeo hayo yatumike na kuleta tija katika maendeleo ya nchi.
THTU imependekeza kuwepo kwa mkakati wa wazi wa kuwashirikisha watunga sera na tafiti ili kuhakikisha kwamba tafiti zinakuwa na majibu ya hoja zilizopo kwenye vipaumbele vya utafiti vya taifa.
Dkt. Loisulie amesisitiza tafiti zisiachwe katika makabati na maktaba bila kujulikana kwa walengwa wa utekelezaji wake.
Hata hivyo amesema pia kuongezeke kiwango cha fedha ambazo zinatengwa kutoka kwenye pato la taifa ili ziende kwenye utafiti Pamoja na Taasisi za elimu ya juu zitakiwe kutenga kiasi fulani cha bajeti zao kwa ajili ya kufadhili tafiti zenye mwelekeo wa maendeleo ya taifa.