Featured Michezo

YANGA SC YAZIDI KUIACHA SIMBA MBIO ZA UBINGWA

Written by mzalendoeditor

Na .Alex Sonna-DODOMA

MABINGWA Watetezi Yanga SC wameendelea na harakati za Kutwaa taji la 29 kwa kuzidi kuiacha Simba SC kwa tofauti ya Pointi 6 baada ya kuichapa mabao 2-0 Namungo FC mchezo wa 22 wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walienda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao moja lililofungwa na beki Dickson Job dakika ya 43 kwa kichwa akiunganisha Mpira wa Kona uliopigwa na Shaban Djuma.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 50 Stephane Aziz Ki alifunga bao la pili baada ya makosa ya Mlinda mlango wa Namungo FC Deogratius Mushi Dida.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 59 na kuendelea kuiacha Simba SC katika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 53 timu zote zikiwa zimecheza mechi 22 huku Namungo FC akibaki nafasi ya sita akiwa na Pointi 29.

About the author

mzalendoeditor