NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MABINGWA Watetezi Yanga wameendelea kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa bao 1-0 Ruvu Shooting mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Ruvu Shooting walijifunga kupitia kwa beki wao wa pembeni Mpoki Mwakinyuke akijaribu kuokoa hatari mbele ya mshambuliaji wa yanga Kenneth Musonda na kutinga moja kwa moja wavuni.Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 56 na kuendelea kuwaacha watani zao Simba katika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 50 wote wakicheza mechi 21.
Mchezo mwingi umepigwa uwanja wa Liti Mkoani Singida wenyeji Singida Big Star wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam KMC watawakaribisha wauaji wa Kusini Namungo FC.