Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao cha Kamati yake na Viongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia taarifa ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum wakati wa Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Januari 23, 2022 jijini Dodoma.
Picha zote na kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM Dodoma
…………………………….
Na WMJJWM Dodoma
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis amesema Wizara inaendelea na utekelezaji wa utatuzi wa changamoto katika masuala mbalimbali yanayoikabili jamii ikiwemo ukatili.
Mhe. Mwanaidi amesema hayo alipokua akijibu hoja katika kikao kazi kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Januari 23, 2023 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mwanaidi ameihakikishia Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge kuwa Wizara itaunda timu itakayoweza kubaini chanzo halisi cha ukatili maana elimu peke yake haitoshi kutatua changamoto hii ya ukatili nchini.
“Tunahitaji kuchukua hatua za haraka zitazotatua changamoto hii kikamilifu ndio maana kama Wizara tumeamua kuja na mbinu hii ya kuunda timu ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tatizo la ukatili katika jamii ” alisema Naibu Waziri Mwanaidi
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mheshimiwa Stanslaus Nyongo ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuhakikisha inashirikiana na Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara zote za kisekta ili kurahisha utatuzi wa janga la ukatili nchini.
“Wizara inabidi ifanyie kazi suala la Udhibiti wa Vitabu vinavyosomwa na Watoto kwani kuna maudhui yanayoharibu na kupotosha watoto na kuchochea ukatili katika jamii kwani vitu wanavyojifunza vinachochea kufanyiana ukatili wao kwa wao“ alisema Nyongo.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara inaendelea kutatua changamoto ya upungufu wa Maafisa Ustawi nchini katika kuhakikisha wanaongeza nguvu katika kupambana na vitendo vya ukatili hasa katika kutoa huduma kwa manusura na wahanga wa vitendo vya ukatili.
“Katika hili la kuongeza Maafisa Ustawi wa Jamii nchini tutashirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza nguvu zaidi katika kupambana na vitendo vya ukatili” alisema Dkt. Chaula
Dkt. Chaula ameongeza Serikali pia inaendelea kuhakikisha inatoanhuduma za Malezi kwa wazee wasio na ndugu kwa kuhakikisha inawapa moyo Maafisa Ustawi wa Jamii wanaowalea Wazee kwani ni kazi ngumu na inayohitaji moyo na wanaifanya kazi hiyo kwa uwezo mzuri.
upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Mpanju ametoa rai kwa Wizara zote za Kisekta kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi ili kutatua changamoto za ukatili unaoendelea nchini.