Featured Michezo

SIMBA SC YAZIDI KUIKABA KOO YANGA MBIO ZA UBINGWA

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna _Dodoma

SIMBA SC wameendelea kuimbiza Yanga katika  mbio za ubingwa baada ya kuichapa Dodoma jiji bao 1_0  Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mshambuliaji mpya kwa mara ya kwanza akiwa amevaa jezi ya Simba SC Jean Baleke alifunga bao dakika 45 +1 baada ya golikipa wa Dodoma jiji kujichanganya na beki wake.

Bao hilo liliwapeleka Simba katika mapumziko wakiwa   mbele kwa bao 1-0 dhidi wenyeji Dodoma Jiji.

Kwa ushindi huo Simba wamefikasha Pointi 50 wakizidiwa Pointi tatu na Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 53 huku wakiwa na mechi moja Mkononi ambapo Simba wamecheza mechi 21.

Mechi nyingine Mbeya City wameibuka na ushindi wa bao 1_0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine jiji Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili kupigwa Singida Big Stars watakuwa uwanja wa Liti Mkoani Singida watawakaribisha Azam FC. 

Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja jioni Yanga SC watakuwa wenyeji dhidi ya Ruvu Shooting kutoka Mkoani Pwani.

About the author

mzalendoeditor