Featured Kitaifa

RC MOROGORO ATETA NA UONGOZI WA TAWA

Written by mzalendoeditor

Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania Ikiongozwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mabula Nyanda wameitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa kwa lengo la Kujitambulisha, na kumpa taarifa zinazohusu Uhifadhi katika Mkoa huo.

Katika salamu hizo, Kamishna wa Uhifadhi alimpatia taarifa ya shughuli mbalimbali ambazo TAWA inafanya katika Pori Tengefu la Kilombero, Fursa na changamoto pamoja na hatua mbali mbali ambazo TAWA imeshachukua katika kukabiliana nazo.

Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe. Fatma Mwasa ameishukuru TAWA kwa kufika ofisini kwake, kumkaribisha vizuri Morogoro, na kuahidi ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo.

“Pamoja na jukumu Lenu kubwa la Uhifadhi Wanyamapori, uwepo wa Makao Makuu yenu hapa Morogoro ni wa msingi sana. Kwani vyanzo vya maji vinakauka, Sababu ya wafugaji wavamizi katika maeneo yenye vyanzo vya maji, Ukataji ovyo wa Miti. Zaidi ya watu milioni 11 wanaoishi hapa na maeneo jirani wanategemea maji ambayo vyanzo vyake ni kutoka Morogoro. Nitashangaa sana kama mtaharakisha kuhamia Dodoma wakati bado mkoa wa Morogoro unawahitaji sana.” Alisema Mhe. Fatma Mwasa.

Kamishna wa TAWA alimkabidhi Mkuu wa Mkoa Nembo ya TAWA na Jarida ambalo lina habari za TAWA.

About the author

mzalendoeditor