Featured Kitaifa

WASABATO SHINYANGA MJINI WAFUNGA SIKU 10 MAOMBI…WALIOMBEA TAIFA

Written by mzalendoeditor
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini, Brian Abdallah (kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi Maalumu.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga mjini limefunga Siku 10 za Maombi Maalumu pamoja na kuombea Taifa Amani  huku likihamasisha binadamu kuthaminiana, kupendana na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Maombi hayo yaliongozwa na Mchungaji Brian Abdallah wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa  Sengerema Mjini Mkoani Mwanza ambayo yalianza Januari 11,2023 na kuhitimishwa leo Jumamosi Januari 21,2023 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini yakiongozwa na Somo lisemalo ‘Kurejea Madhabahuni’.
 
Akiongoza Maombi ya kufunga Siku 10 za Maombi wakati wa Ibada leo Jumamosi Januari 21,2023, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini, Brian Abdallah amesema maombi hayo yamekuwa na baraka nyingi.
 
“Maombi haya ya siku 10 za mfungo yamekuwa na muitiko mkubwa awali tulikuwa ndani ya Kanisa lakini watu walikuwa wengi ikabidi tuhamie nje ya Kanisa, na watu wote wamebarikiwa,”amesema Mchungaji Brian.
 
Amesema katika siku hizo 10 za mfungo wa maombi, pia wameliombea Taifa kuendelea kuwa na amani, ikiwemo kukoma kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na mauaji.
 
“Tumemuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri, Wabunge, Madiwani na viongozi wote. Tunataka nchi hii iendelee kuwa na amani, watu waishi kwa amani na upendo, wathaminiane na kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema Mchungaji Brian.
 
“Kumekuwa na matukio ya ukatili yanatokea katika jamii mfano mme anaua mke wake,tunalaani matukio haya na hatupendi kuyasikia, naomba binadamu tuwe na upendo. Ni lazima tuwe na upendo ili jamii iishi kwa amani. Eee Mwenyezi Mungu ingilia kati vitendo vya mauaji yanayoendelea katika jamii, komesha ukatili wa kijinsia ukalete amani na utulivu”,amesema Mchungaji Brian.
 
Kwa upande wake Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini amewaomba viongozi wa dini kote nchini kuongeza kufundisha waumini wao kuishi kwa kuthaminiana na kupendana pamoja na jamii kumrudia Mungu ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia nchini.
 
Na baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo akiwemo Elizabeth Kasuka na Tumaini Nduta, wamesema katika siku hizo 10 za maombi wamebarikiwa na bwana, na kutoa wito kwa Watanzania wamrudie Mungu na kuacha kufanya vitendo viovu.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa mbele sehemu ya Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah (kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi.

Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini

Maombi Maalum kuliombea Taifa yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada

Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi

Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi Maalum katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor