Featured Kitaifa

NABII DKT GEODEVI ATOA MILIONI 100 SOKO LA SAMUNGE ASISITIZA KUWA HATAFUTI WAFUASI 

Written by mzalendoeditor
Askofu  wa huduma ya Ngurumo ya Upako Nabii mkuu Dkt Geordevi Kasambale akiongea wakati alipotembelea soko la machinga la Samunge Jijini Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo akiongea na wafanyabiashara wa soko la Samunge jijini Arusha
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la machinga la Samunge wakifuatilia jambo Nabii Mkuu Geordevi Kasambale wa huduma ya Ngurumo ya Upako alipotembelea soko hilo.
……………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Askofu wa kanisa la Ngurumo ya Upako Nabii mkuu Dkt Geor Devid Kasambale ametoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa wafanyabiashara wa soko la wamachinga la Samunge jijini Arusha kwa lengo la kuwasaidia mitaji pamoja ukarabati wa soko.
Akikabidhi fedha hizo katika ziara yake ya kutembelea soko hilo alisema kuwa alipokea barua ya kuomba msaada  ambapo ameona ni vema kuwashika mkono  kwa kurudisha alichonacho kwa jamii  ambapo ameguswa kuwasaidia kwa kuwapa mitaji midogo midogo kulingana na mahitaji yao.
Dkt Geordevi alisema kuwa ametoa msaada huo sio kwasababu anatafuta wafuasi au anataka kubadilisha watu dini zao bali ni kwakuwa ameguswa kuwasaidia kwani vijana na akina mama wanateseka kutafuta riziki kutokana na ukosefu wa mitaji.
“ Sibagui mtu Mimi ni nabii wa watu wote hata wabagani  kwahiyo katika utoaji wa fedha hizi mtu asikuambie wewe hupati kwasababu huendagi Ngurumo ya Upako Wala wewe sio mkristo hapana nimesaidia watu wote wa soko hili wenye mahitaji mimi sitafuti waumini wala sipo hapa kubadilisha mtu dini,” Alisema Dkt Geordevi.
“Tutakuwa tunashirikia kwenye kila hitaji kwani kinachonisukuma kusaidia jamii ni kwasababu  nilipewa wajibu wa kuleta injili kwa maneno na baadae Mungu alinitaka kubadilisha na kuleta injili kwa vitendo na ndicho ninachokifanya sasa,” Alieleza.
Aidha amewataka viongozi wa dini nchini kujenga tabia ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa kile kinachopatikana katika Taasisi zao ili kupunguza mzigo kwa serikali kushughulikia mahitaji madogomadogo ikiwemo mikopo kwa wajasiriamali.
Alisema kuwa haina haja ya viongozi wa dini kujilimbikizia fedha ikiwa watu wengine wanakosa hata chakula kwani wapo watu wanateseka kwa shida na ikumbukwe haohao ndio waliowanuinua wao.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo akisalimia wananchi wa eneo hilo  kabla ya nabii huyo kuongea na wafanyabiashara hao alisema wakati nabii huyo akiandaa ziara hiyo sokoni hapo kunamaneno maneno yaliibuka
Aliongeza kuwa kunawatu wanakereka sana Geordavie kuitwa Nabii Mkuu na yeye anamuita Nabii Mkuu kwasabababu anaheshimu kipawa alichopewa nabii huyo.
Alisema katika soko hilo kunamambo matatu yanayolikabili na mwaka 2019 soko hilo liliungua na hakukuwa na msaada wowote bali wajasiriamali hao waliishi kwa changamoto hizo kwa muda mrefu ikiwemo mitaji.
Alisema soko hilo linachangamoto za mitaro,majengo ikiwemo usumbufusumbufu wa migambo na waliposikia unakuja hapa kunabaadhi ya migambo walichukua vitu vya wafanyabiashara hao.
“Kunabaadhi ya mambo niliyafanya sokoni hapa ikiwemo kisima Cha maji na nilitoa sh,milioni 20 kwakinamama 100 kunawengine walirudisha na wengine waliweza kurudisha namuachia mungu”
Aliahidi kutoa sh,milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa soko hilo na hakuna mtu atakayepewa hela mkononi lakini soko hili lipo chini ya halmashauri tutakaa vikao na madiwani wenzangu ili tubadilishe soko hili ili liwe la kisasa kwanibaadhi ya Wataalam wakipelekewa hoja ya soko hilo kubadilika wanapingapinga tu hivyo ukiwaombea watabadilika “
Alisema anatambua jinsi anavyokomboa watu mbalimbali,mitaji,fedha,pikipiki na hiyo ndio maana ya utumishi wa mungu kwani anachovuna ndicho anachokula na watumishi wake.
Gambo alitahadharisha fedha hizo ziwafikie wanyonge kwani zimeombewa hivyo walengwa wataotafutwa wawe ni watu wafanyabiashara wa soko hilo kwelikweli kwani hela hiyo inaupako iachiwe iguse maisha ya watu
Diwani wa Kata ya Kati,Abdulrasul Tojo alimpongeza Nabii Geordavie kufika eneo hilo na madiwani hao waliomba kwa pamoja kurodhia soko la Samunge kuwa chini ya nabii huyo
Alisema soko hilo baada ya kuungua miaka mitatu iliyopita wafanyabiashara waliunguliwa bidhaa zao eneo hilo na hadi sasa halijajengwa
“Tunaomba ukiwezekana madiwani waridhie soko hili liwe chini yako kwani wajasiriamali hawa wanahitaji furaha na amani kutoka kwa watu mbalimbali hivyo madiwani naomba mridhie soko  hil likiwa chini yako”
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Ofisa Tarafa wa tarafa ya Themi hiyo Chausiku Baha alisema yeye kama ofisa tarafa huyo atawasiliana na nabii huyo ili kuzitatua”
 Mwakilishi wa Wafanyabiashara hao , ambaye ni katibu wa Afya Soko la Samunge  Loveness Joakim  akisoma risala  Alisema soko hilo lilianzishwa 12 Septemba mwaka 2012 likiwa na jumla ya vibanda 2106 likiwa na wafanyabiashara 2,106
Joakim wafanyabiashara hao wanajihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali na lipo chini ya halmashauri ya Jiji la Arusha na Machi 28 mwaka 2019 soko hilo liliungua na bidhaa ziliungua huku mitaji ikiungua.
Alisema soko hilo halina mageti ya kutosha na ujio wake nabii huyo utawezesha wafanyabiashara kujikwamua kiuchumi na kujipatia mahitaji yao.

About the author

mzalendoeditor