Featured Kitaifa

WAZIRI DKT. JAFO AFANYA IARA JIMBONI KISARAWE

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu

Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ambaye pia ni
Mbunge wa Kisarawe leo Januari 14, 2023 amefanya ziara Kata ya Boga jimboni humo.

Mhe. Dkt. Jafo amelishukuru Shirika la Direct Aid kwa ushirikiano uliotukuka kwa Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe.

"Direct Aid mmefanya vitu vingi kisarawe, mmetoa solar power, hili la kutujengea zahanati ni jambo
kubwa tutaonesha nasi ushirikiano wa kutosha katika masuala ya afya, elimu na ushirikiano katika
ufugaji wa mbuzi na ng'ombe," alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Direct Aid Bw. Mohamed Orab alisema tangu walipoingia wilayani humo
mwaka 2020 wameendelea kushirikiana vyema na wananchi na kuwa wapo tayari kuanza Ujenzi wa
Zahanati ya Boga.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kisarawe Ndg. Peter Ngussa
amelishukuru shirika hilo akisema kujengwa kwa zahanati hiyo itakuwa mwarobaini wa changamoto
kwa wananchi.

Aidha, Diwani wa Kata ya Boga Mhe. Inadi Chakachaka ameshukuru sana msaada huo wa ujenzi wa
zahanati kwani utawapunguzia wanawake wa kata hiyo umbali wa kwenda kutibiwa ktk Kituo cha
Afya Maneromango.

About the author

mzalendoeditor