Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AIAGIZA TFS KUPITIA UPYA UTARATIBU WA  UTOAJI LESENI ZA UKATAJI MITI

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Wananchi pamoja na Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akipata akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru kabla ya kuanza kupanda miti  kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12, 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Mdodoma kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango akishuhudia baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma wakipanda mti aina kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati alipoongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Ihumwa  mara baada ya kumaliza zozezi la upandaji miti kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati alipoongoza zoezi la upandaji miti hiyo kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Msabuni katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo  wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent  Bashungwa  wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Wakuu wa wilaya Mkoa wa Dodoma  wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato  wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Mabalozi wa Mazingira  Mkoa wa Dodoma  wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Wananchi pamoja na Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

 Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda ,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent  Bashungwa,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato  Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji Mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

…………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango, ameuagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kupitia upya utaratibu wa leseni za ukataji miti kwa ajili ya mkaa ili kuokoa maeneo ambayo yana uoto na vyanzo vya maji.

Dk.Mpango,ameyasema hayo jijini Dodoma  mara baada ya kumaliza kupanda mti katika shule ya msingi Msalato, tukio lililoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Januari 12,2023.

Amesema kuwa TFS lazima  mkapitie upya utaratibu huu wa utoaji wa leseni za ukataji miti kwa ajili ya mkaa kwani hivi sasa hali ni mbaya sana kama pale Mzakwe ambapo ndipo chanzo kikuu cha maji kwa jiji la Dodoma.

“Kila nikipita barabarani nasikitika sana unakuta misururu ya magunia ya mkaa na shughuli za ukataji miti zikiendelea sasa itafika wakati miti yote ikiisha kule mlimani ambapo ndiko eneo muhimu kwa ajili ya vyanzo vyetu vya maji vitakauka mara moja”amesema Dk. Mpango

Hata hivyo Dkt. Mpango amesema kwa sasa suala la upandaji miti linapaswa kuwa la lazima na kuziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafikia lengo la upandaji miti milioni moja na laki tano kwa mwaka kama ilivyopangwa.

”Ushirikishwaji wa sekta binafsi na wafanyabiashara katika upandaji na utunzaji miti pamoja na kuzisihi familia kuongeza juhudi katika upandaji miti na usafi wa mazingira. Pia amezitaka taasisi za serikali kupanda miti katika maeneo yao na kuhakikisha miti hiyo inaishi.”amesisitiza Dk.Mpango

Aidha  ameagiza Jiji la Dodoma kuratibu zoezi la usimamiaji miti iliopandwa ili kuhakikisha inaishi na kupendezesha jiji.

Dkt. Mpango ametoa wito kwa Waandishi wa Habari hapa nchini kutoa kipaumbele katika kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya upandaji miti na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla.

”Ni muhimu kwa waandishi wa Habari kutoa habari za mifano ya wale walioweza kutunza mazingira ili wawe hamasa kwa watanzania wengine.”amesema Dk.Mpango

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema tayari mipango mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira imeanza kutekelezwa ikiwemo kugawa maeneo yaliopandwa miti  kwa taasisi za serikali na binafsi ili waweze kusimamia na kuhakikisha miti hiyo inaishi.

Waziri Jafo amemuhakikishia Makamu wa Rais zoezi la upandaji miti na kuitunza miti hiyo litakua endelevu wakati wote.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda ametoa wito kwa wananchi kuzingatia utaratibu wakati wa upandaji wa miti ikiwemo kuandaa mazingira ya upandaji na kufuata maelekezo ya wataalamu ili kufahamu aina ya mti na mahali unapopaswa kupandwa.

”Jiji la Dodoma linakabiliwa na upungufu wa mvua hivyo ni vyema uchimbaji wa mashimo pamoja na nafasi baina ya mti na mti ukawa wa kitaalamu zaidi ili kuepusha miti hiyo kutofikia lengo. ”ameeleza Mhe.Pinda

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema upandaji miti katika vyanzo vya maji umepewa kipaumbele mkoani Dodoma kwa kuanza na Bonde la Mzakwe ambalo limekua na changamoto ya ukuaji wa miti.

Amesema tayari wataalamu wamewezesha aina ya miti inayopaswa kupanda pamoja na kuweka mazingira yatakayookoa miti hiyo dhidi ya hatari ya moto.

About the author

mzalendoeditor