Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akipanda miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba,akipanda miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru ,akipanda miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph ,akipanda miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru mara baada ya kupanda miti eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi wakati wa zoezi la la upandaji miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wakati wa zoezi la la upandaji miti katika eneo la Tambukareli jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
…………………………………..
Na Bolgas Odilo-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo ameuagiza wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA na wakala wa barabara nchini TANROADS kuhakikisha wanatekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kuzingatia upandaji miti kandokando ya barabra hizo.
Waziri Jafo ametoa maagizo hayo leo Januari 10,2023 jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Tambukareli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Waziri Jafo amesema kuwa wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) wahakikishe wanapanda miti kandokando ya barabara zilizopo katika maeneo mbalimbali ili mazingira yaendelee kutunzwa.
”Nataka viongozi wa majiji na manispaa kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijiji na Vijijini (TARURA) kupanda miti ya kutosha kandokando ya barabara zinazopopita katika maeneo yao ili kuhifadhi mazingira.”amesema Dkt.Jafo
Vile vile, amesema kuwa kuelekea maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu matukio ya upandaji miti yataendelea ili kuhifadhi mazingira.
“Lazima tupande miti ili kuifanya Dodoma ya kijani na hii kampeni ya kukijanisha mkoa huu ilizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa makamu wa Rais mwaka 2017”amesisitiza Dkt. Jafo
Hata hivyo amewasisitiza wakuu wa shule nchini kuhakikisha wanafunzi wote wanaojiungana na shule hizo kupewa miti ili wapande kila mmoja. kidato cha kwanza wanapanda miti.
”Nataka wakuu wa shule nchini kuhakikisha kila mwanafunzi anayeandikishwa shuleni anapewa mti mmoja wa kupanda ili kuendana na Kampeni ya ‘Soma na Mti’ ambayo inalenga kupanda miti zaidi ya milioni 14.5.”amesema Waziri Jafo
Aidha Waziri Jafo amewataka wataalamu wa kilimo wabainishe aina za miti ipandwe katika maeneo gani ili kuepuka changamoto ya baadhi ya miti kufa.