Featured Michezo Uncategorized

AZIZ KI AING’ARISHA YANGA UGENINI

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo

MABINGWA Watetezi Yanga SC imeumaliza mwaka kwa ushindi baada ya kuwachapa wenyeji Mtibwa Sugar bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika uwanja wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro.

Yanga walipata bao kunako dakika ya 26 likifungwa na Stephane Aziz Ki  kwa faulo ya moja kwa moja iliyomshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar baada ya Kibwana Shomari kuchezewa rafu.

Kwa ushindi huo Yanga  SC wamefikisha Pointi 50 na kuwaacha watani zao Simba SC kwa tofauti ya Pointi 7 ,Simba wakiwa nafasi ya pili wakiwa na Pointi 44.

About the author

mzalendoeditor