Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AZINDUA KITUO KIKUU CHA POLISI RUANGWA

Written by mzalendoeditor

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa kwanza kulia) akifungua kitambaa kuashirikia uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022. kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Hassan Ngoma (kulia), Wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi Hassan Jarufu (wa pili kushoto)  na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ruangwa Ibrahim Ndoro (kushoto)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Polisi Mhandisi Fadhili Majid Ishekazoba (wa tatu kulia) wakati wa  uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022. kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack, 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022. kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack (Kulia). Wengine ni  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi Hassan Jarufu, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ruangwa Ibrahim Ndoro na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Hassan Ngoma (wapili kulia) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua moja ya chumba wakati alipozindua Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022. Kamishna Msaidizi wa Polisi Mhandisi Fadhili Majid Ishekazoba (kulia) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akimkabidhi Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, pikipiki mbili ambazo zitatumiwa na Polisi wilaya ya Ruangwa katika kutekeleza majukumu mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi Disemba 31, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack 

Muonekano wa  Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa ambacho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekizindua Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, kilichopo Ruangwa Mkoa wa Lindi, Disemba 31, 2022. 2022 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kituo Kikuu cha Polisi cha wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na amesema kuwa jengo hilo linalenga kuboresha utendaji wa polisi hususani katika ulinzi wa raia na mali zao.
Amezindua jengo hilo leo (Jumamosi, Desemba 31, 2022) ambapo amesema mbali na kuboresha utendaji wa polisi pia jengo hilo litawarahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi na kuwapunguzia gharama za kutembelea umbali mrefu kufuata huduma.
Kadhalika, Mheshimiwa Waziri Mkuu amekabidhi pikipiki mbili kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kwa ajili ya kituo hicho pamoja na kituo kidogo cha Ndagala. Ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 190.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 99 na kwamba katika mwaka ujao wa fedha wizara inakusudia kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za awali za askari wa kituo hicho.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ifanye maboresho ya makazi ya askari katika mkoa huo ili waweze kuishi katika mazingira bora Zaidi yatakayowawezesha kutekeleza majuku yao ipasavyo.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekabidhi pikipiki 25 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ruangwa ili ziweze kuwasaidia makatibu wa kata katika kufuatilia utekelezaji wa Ilani.

About the author

mzalendoeditor