Featured Michezo

BILA FEI TOTO,YANGA YAIZAMISHA AZAM FC

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo-MZALENDO BLOG

MABINGWA Watetezi Yanga wameendelea kugawa dozi katika Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuwachapa matajiri wa Chamazi Azam FC mabao 3-2 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdul Sopu dakika ya 27 akimalizia pasi ya Prince Dube huku Yanga wakipata mabao kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 31 na Stephane Aziz Ki dakika ya 33 na kuenda mapumziko Yanga wakiwa wanaongoza.

Kipindi cha pili Azam FC walipata bao la mapema dakika ya 47 likifungwa na Abdul Sopu na bao la ushindi la Yanga likifungwa na Farid Mussa dakika ya 78.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 47 na kuiacha Azam FC kwa tofauti ya Pointi 10 huku wakicheza bila kiungo wao Fei Toto anayedaiwa kusajiliwa na Azam FC.

About the author

mzalendoeditor