TIMU ya Taifa ya Argentina wametangazwa kuwa Mabingwa wa Kombe la Dunia 2022 baada ya kuifunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 120 wakifungana 3-3. Mechi hii inakuwa ya mwisho Kombe la Dunia kwa staa wa Argentina Lionel Messi.