Featured Kitaifa

WIZARA YA AFYA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA HOSPITAL YA RUFAA KATAVI KUANZA KUTOA HUDUMA ZA TIBA 1 JANUARI 2023

Written by mzalendoeditor

Kufatia maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa jana tarehe 12/12/2022 katika ziara yake ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi aliagiza kuhakikisha huduma za tiba zinaanza kutolewa ifikapo tarehe 1 Januari, 2023 katika Hospitali hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abeli Makubi amekutana mara moja na wakandarasi na menejimenti ya Hospitali hiyo, kuhakikisha kuwa wanaweka mpango harakishi wa kukamilisha jengo la Wing A kabla ya tarehe 30/12/2022.

Katika Kikao hicho, Prof. Makubi ameelekeza kila mdau katika mradi huo afanye kazi usiku na mchana bila kuathiri ubora wa huduma na amepanga kurudi kukagua utekelezaji wake kabla ya tarehe 24 Desemba, mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor