Featured Kitaifa

MAJALIWA AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KUKAMILISHA UJENZI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KATAVI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA AFYA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KATAVI

Na. Majid Abdulkarim, WAF- KATAVI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kasim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Afya kwa kutekeleza maagizo ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi ambapo kwa sasa imefikia asilimia 92

Mhe Majaliwa ametoa pongezi hizo leo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo amekuta kunaongeza la kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kutekelezwa maagizo yake ya kushirikiana na ofisi ya Mkoa katika kusimamia mradi huo, Maagizo hayo aliyatoa mwaka jana 2021 mwezi wa nane.

Mhe. Majaliwa ametembelea Hospitali hiyo na kukuta ujenzi umefikia asilimia 92 kwa Wing A kutoka asilimia 40 mwaka jana.

Aidha Mhe. Majaliwa amemuagiza Meneja TANESCO Mkoa wa Katavi kufikia Tarehe 23 Desemba mwaka huu kuwa amepeleka umeme katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ili kuwezesha huduma za awali kuanza kupatika.

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof Abel Makubi alitoa taarifa kuwa mradi wa Wing A utakamilika tareh 31 Disemba 2022 na huduma zitaanza kutorea tarehe 01 Januari 2023 na Ujenzi wa Wing B unategemea kukamilika Oktoba 2023.

Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi umefikia asilimia 92 na zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 9 .2 kimeshatolewa na serikali kati ya bilioni 12.3”, ameeleza Prof. Makubi

Prof Abel Makubi amesema Hospital zote za Mikoa nchi nzima zitapatiwa site scan kwa ajili ya kutoa huduma ya mionzi kwa wananchi

Pia ameeleza kuwa Hospitaal ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi itakapo kamilika wingi A mwishoni mwa mwaka huu itakuwa na uwezo wa kulaza Wagonjwa 170 kwa wakati mmoja.

About the author

mzalendoeditor