Featured Kitaifa

JAMII YATAKIWA KUENDELEZA MSINGI WA VIJANA KUJA NA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA JAMII.

Written by mzalendoeditor
Meneja wa mradi wa Future STEM Business Leaders Josephine Sepeku akiongea na waandishi wa habari juu ya mradi huo.
WANAFUNZI wakielezea bunifu walizozileta katika mashindano hayo 
WANAFUNZI kutoka shule ya sekondari ya Arusha girls wakiwa pamoja na kifaa walichokibuni kinachosaidia katika usafi wa mazingira.
PICHA ya pamoja ya wanafunzi kutoka shule saba za mkoa wa Arusha walioshiriki katika mradi wa Future STEM Business Leaders pamoja na viongozi washiriki wa mradi huo.
…………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Jamii imetakiwa kuendeleza msingi wa vijana kuja na suluhu ya changamoto zilizopo katika nchi msingi ulioanzishwa na mradi wa Feature stem business leaders ikiwa ni pamoja na kubadilisha thamani ya elimu kuwa zao na huduma.

Rai hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi- COSTECH Dkt Erasto Mlyuka  katika mashindano ya kushindanisha shule saba za mkoa wa Arusha  katika bunifu walizoziandaa zenye kutatua changamoto katika jamii kupitia mradi unaofanywa na taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)  na chuo kikuu Dar es salaam.
Dkt Mlyuka alisema kuwa mradi huo ulikuja baada ya institution ya taasisi ya Phizikia ya uingereza kuona Kuna changamoto katika Dunia kuwa wanafunzi wengi hawapendi masomo ya sayansi badala yake wanakimbilia kwenye masuala ya biashara na jammii haiwezi kufanya biashara bila kuwa na vitu vinavyotokana na masomo ya kisayansi.
“Leo hapa Arusha tumeona vijana wamekuja na suluhu ya changamoto tulizonazo kuna waliokuja na suluhu ya kimazingira na wengine mbolea sasa ni lazima mawazo kama haya tuendelee kuyalea ili yaje kutengeneza viwanda  kwani chochote kinachofanya kazi leo chanzo chake kilikuwa ni wazo,” Alisema Dkt Mlyuka.
Alifafanua kuwa wameonesha sampuli  kifaa ambayo inaweza isitatue changamoto za hapa nchini tuu bali Dunia  nzima na wapo kwenye hatua ya kuhakikisha mfumo wa programu hiyo unaohusisha Mwalimu, Mwanafunzi na mtaalamu wa biashara ambaye yupo sokoni unaendelezwa nchi nzima.
“Niwapongeze wanafunzi wote, mmeanza safari ya ubunifu, hamtakaa mlale, ubunifu unahitaji kujitoa, kujali wengine na kujituma kwahiyo naamini zawadi mlizozipata na vyeti mlivyotunukiwa vitawakumbusha na kuwafanya mjione kumbe mnaweza,” Alisema.
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC) Dkt Musa Chacha alisema kuwa ni vema mradi huo umeona Phizikia kama fursa kwani tatizo kubwa ni maarifa ambayo wanawapatia watoto ambayo wasipo tafsiri vizuri Mwanafunzi atapata A darasani lakina haina maana katika maisha yake.
Kaimu mkuu wa chuo ATC Dkt Yusuph Mhando alisema taifa lina tatizo la ajira kwa vijana na suluhisho ni bunifu za kisayansi zilizofanyika katika mashindano hayo ambapo yakiendelezwa yatatoa suluhu ya changamoto zilizopo katika jamii pamoja na kutoa ajira kwa vijana.
Kwa upande wake Meneja wa mradi wa Future STEM Business Leaders Josephine Sepeku alisema kuwa mradi huo  unalenga kujenga na kutatua changamoto za biashara pamoja na sayansi ambapo wanafundisha  wanafunzi wanaosoma sayansi kutumia sayansi za darasani kuzileta katika mfumo wa biashara na wanapitia hatua mbalimbali ikiwemo za kuwa wabunifu wa kutengeneza vitu vinavyotatua changamoto zilizopo katika jamii.
“Tunaposema vijana wajiajiri, tunaposena Tanzania ya viwanda tunaanzia hapa, tunawapatia mafunzo ili wao waweze kutengeneza na leo tumekuwa na shule saba ambazo zimeweza kushiriki, wanafunzi wakiwa ni 35 na wameweza kuja na bunifu mbalimbali na tumeweza kupata washindi watu,” Alieleza.
Alieleza kuwa mshindi wa kwanza ni shule ya Arusha girls ambao wamekuja na kifaa cha utunzaji wa mazingira, ambapo inaleta usafi wa mazingira lakini pia kuleta biashara kutokana namkaa unaotoka katika kifaa hicho baada ya taka kuwekwa unaweza kutengenezewa matofali.
Alisema mshindi wa pili ameweza kuleta suluhu ya changamoto tunazokutana nazo kama vile barabarani kwa kuja na mfumo unaoweza kupunguza ajali zinazotokea kutokana na kutokuelewa maeneo ya barabara au kutokufuata sheria  pamoja  na mshindi wa tatu ambaye ameweza kutengeneza mbolea isiyo na kemikali.

About the author

mzalendoeditor