Featured Kitaifa

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WAMETEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA KATIKA NCHI YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU ULIPO ABU DHABI

Written by mzalendoeditor

Kaimu Balozi wa Tanzania katika Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E), Mheshimiwa Idd Seif Bakari akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti shughuli zinazofanywa na ubalozi wa Tanzania nchini humo wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za ubalozi huo zilizopo Abu Dhabi, Kamati ya Bajeti inafanya ziara nchini humo kujifunza masuala mbalimbali ya kibajeti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Daniel Sillo akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) iliyopo Abu Dhabi na kukutana na Kaimu Balozi Mheshimiwa Idd Seif Bakari na maafisa wengine wa ubalozi huo, Kamati ya Bajeti inafanya ziara nchini humo kujifunza masuala mbalimbali ya kibajeti

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania katika Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mheshimiwa Idd Seif Bakari na maafisa wengine wa ubalozi huo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo iliyopo Abu Dhabi, Kamati ya Bajeti inafanya ziara nchini humo kujifunza masuala mbalimbali ya kibajeti

PICHA NA OFISI YA BUNGE

About the author

mzalendoeditor