Featured Kitaifa

YANGA YAISHUSHA TENA SIMBA SC

Written by mzalendoeditor

MABINGWA Watetezi Yanga wameishusha kileleni Simba SC baada ya kuichapa bao 1_0 Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Shujaa wa Yanga ni Kiungo Mshambuliaji Fei Toto ameokoa timu yake dakika za lala salama 89 akifunga bao kwa pasi ya Farid Mussa.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 14,nafasi ya pili Simba wakiwa na Pointi 34 wakicheza mechi 15.

About the author

mzalendoeditor