Kitaifa

BALOZI FATMA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI MDOGO WA CHINA

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Mdogo wa China uliopo Mazizini – Zanzibar, kufuatilia kifo cha Rais Mstafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin kilichotokea Novemba 30, 2022. 

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Balozi Fatma ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Watu wa China na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na kiongozi wao mpenda amani, maendeleo na ustawi wa jamii yake.

Rais huyo wa zamani alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 96, Pia Jiang aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China kuanzia 1989 mpaka 2002 alichukua madaraka kutoka kwa Zhao Ziyang. Jiang atakumbukwa kwa kuwa kiongozi hodari na kuwa mwanzilishi wa kutaka kufanya mapinduzi ya kiuchumi hatua ambazo zimezaaa matunda na kupatikana kwa China moja na yenye maendeleo.

Serikali ya Tanzania na Watanzania wake kwa ujumla wanaungana na Serikali ya Watu wa China kuombeleza musiba huo mzito.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Mdogo wa China uliopo Mazizini – Zanzibar, kufuatilia kifo cha Rais Mstafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyika Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng baada ya kumaliza kutia saini kitabu cha maombelezi kufuatilia kifo cha Rais Mstafu wa Jamhuri ya Watu wa China Jiang Zemin
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyika kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng pamoja na Mkurugenzi wa Ofisi za Mambo ya Nje Zanzibar, Bi. Mariam Mrisho baada ya kumaliza kutia saini kitabu cha maombelezi kufuatilia kifo cha Rais Mstafu wa Jamhuri ya Watu wa China Jiang Zemin

About the author

mzalendoeditor