RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Dk. Kiva Mvungi (kulia) cheti kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kupitia Mfuko wa UKIMWI wa Taifa (AIDS Trust Fund).
GGML imepokea zawadi hiyo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo tarehe 1 Disemba, 2022 mkoani Lindi. Kampuni hiyo imeahidi kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kupitia Kampeni ya Kili Challenge.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa na GGML miaka 20 iliyopita na inalenga kuongeza uelewa pamoja na kukusanya fedha za mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI.