Featured Kitaifa

MLINZI WA KAMPUNI BINAFSI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI.

Written by mzalendoeditor

Mnamo tarehe 28.11.2022 majira ya saa 05:30 asubuhi huko maeneo ya Benki ya Azania jengo la NHIF lililopo Kata na Tarafa  ya Sisimba, Jijini Mbeya,  Mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya suma JKT aitwaye OSEA S/O MAGAISHA @ KASHIRIRIKA [21] Mkazi wa Makunguru alifariki dunia  baada ya kujiua kwa kujipiga risasi sehemu ya shingo kwa kutumia silaha aina ya shot gun pump action yenye namba 00715v mali ya suma JKT akiwa lindoni Benki ya Azania.

Chanzo cha tukio hili kinachunguzwa. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Vielelezo ambavyo ni bunduki moja aina ya shot gun pump action yenye namba 00715v, risasi 04 za shot gun na ganda moja la risasi ya shot gun vimehifadhiwa kituo cha Polisi kwa uchunguzi zaidi.

Imetolewa na:

Abdi Issango – ACP

Kaimu Kamanda wa Polisi

Mkoa wa Mbeya.

About the author

mzalendoeditor