Featured Kitaifa

MKURUGENZI MTENDAJI UNAIDS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UKIMWI (UNAIDS), Bi. Winnie Byanyima amewasili nchini tarehe 27 Novemba , 2022. 

Mkurugenzi huyo atakuwepo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi kuanzia Tarehe 28 Novemba hadi 6 Desemba, 2022.  Mara baada ya kuwasili nchini, Bi. Byanyima alipokelewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel

Akiwa nchini Bi. Byanyima atashiriki Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Mkoani Lindi pamoja na kushiriki uzinduzi wa taarifa ya Hali ya Ukimwi nchini pamoja na kukutana na Baraza la watu wanaoishi na VVU (Nacopha). 

Aidha, Bi. Byanyima, anatarajia kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Mapinduzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UKIMWI (UNAIDS), Bi. Winnie Byanyima akiwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba , 2022

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UKIMWI (UNAIDS), Bi. Winnie Byanyima baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba , 2022

About the author

mzalendoeditor