Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724(Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya Kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724(Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili Wimbo wa Taifa na Ule wa Afrika Mashariki kabla ya Kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724(Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi zawadi Maafisa Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa hao 724 kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Wanafunzi mara baada ya Kuwatunuku Kamisheni kwa Cheo cha Luteni Usu kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani 

Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Maafisa wa Juu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye Sherehe za Kamisheni kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Shahada ya Sayansi ya Kijeshi Wahitimu 109 kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa zawadi Wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha 

WAHITIMU

Mhe. Rais akifunga

…………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 03/19 wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na kundi la 69/21 Refu.

Akitoa maelezo katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi (TMA) Monduli, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Brig. Jen. Jackson Mwaseba amesema kati ya wanafunzi waliohitimu wanawake ni 89 na wanaume 635.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Cairo Mwaitete amesema JWTZ imekuwa ikishirikiana na Chuo hicho kutoa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi ambapo kwa kipindi cha miaka 3 ya ushirikiano jumla ya wanafunzi 313 wamehitimu.

Aidha, Dkt. Mwaitete amesema Shahada hiyo inawaandaa maafisa waliohitimu kuweza kuwa mahiri katika kusimamia masuala ya kijeshi, amani pamoja na uongozi kiuchumi, kisiasa na kijamii. 

Dkt. Mwaitete pia amesema Chuo cha Uhasibu kina mpango wa kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa Shahada mbalimbali zikiwemo usalama wa mitandao, usalama na masomo ya kimkakati, masomo ya ulinzi na amani pamoja na ulinzi wa taarifa 

Hali kadhalika, Dkt. Mwaitete amesema Chuo cha Uhasibu kinaunga mkono mpango wa Serikali kupeleka Vyuo vya Elimu ya Juu katika mikoa ya pembezoni kupitia fedha za Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Pamoja na kutunuku Kamisheni, Mhe. Rais Samia ametoa zawadi kwa Maafisa wanafunzi waliofanya vizuri katika mafunzo hayo.

About the author

mzalendoeditor