Featured Kitaifa

DK. JAFO MHITIMU BORA ALIYELETA MANUFAA KWA CHUO NA TAIFA MIAKA 40 YA SUA

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipokea Tuzo ya kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akionesha Tuzo ya kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) baada ya kutunukiwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea Tuzo ya kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Tuzo iliyotolewa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ya kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

………………………..

Kuelekea miaka ya 40 ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimetoa tuzo ya kuthamini mchango mkubwa wa Mwanafunzi aliyewahi kuhitimu katika chuo hicho mnamo mwaka 2001, Dk.Selemani Jafo ambaye alifanya vizuri katika masomo yake na kuleta mchango mkubwa kwa jamii.

Dk. Jafo amekuwa miongoni mwa wanazuoni wachache waliosoma SUA kupata tuzo ya aina hiyo kwa miaka tofauti tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Chuo hicho kimekuwa kikifuatilia mwenendo na tabia za wanazuoni wao waliohitimu chuoni hapo ili kubaini mchango wao katika jamii.

Katika Tuzo hiyo, Dk.Jafo kutokana mchango mkubwa alipokuwa katika nafasi ya mtaalam wa kilimo wa Halmashauri ya Kisarawe kwa mwaka 2001 hadi 2005. Pia taarifa ya chuo hicho imeonyesha kwamba Dk. Jafo alikuwa Mtanzania wa kuigwa kwa kuchapa kazi kwa kuleta matokea alipokuwa akifanyakazi katika shirika la Kimataifa la Plan International ofisi ya Tanzania kwa nafasi ya Meneja wa Miradi.

Katika nafasi ya ubunge Dk. Jafo amehudumia vyema wananchi wake sambamba na kuliwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la SADC ikiwa ni pamoja na kuwa Mweka hazina wa bunge hilo la SADC kwa matokeo chanya. Eneo lingine kubwa lililompa heshima hiyo ni kuwa kiongozi mwenye ari, mnyenyekevu, na anaye jituma kwa moyo mkubwa bila ya kuchoka kwaajili ya jamii alipokuwa Waziri wa TAMISEMI na katika nafasi yake ya sasa ya waziri wa Muungano na Mazingira.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Dk. Jafo amesema “Hii ni heshima kubwa Sana kwake, familia yangu, na taifa langu. Pia natoa Shukran za dhati kwa Uongozi Chuo kikuu cha Kilimo SUA Kwa kunipatia Tuzo hii kwa maana nilipata kusoma hapa miaka iliyopita katika ngazi ya Shahada na Wanafunzi wapo wengi Sana ila waliona wanipatie mie hasa kwa Mchango mkubwa nilioutoa katika nyanja mbalimbali katika jamii.”

About the author

mzalendoeditor