Featured Kitaifa

RC SENDIGA: JAMII YA RUKWA IMENUFAIKA NA MRADI WA LISHE ENDELEVU

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa USAID/Lishe Endelevu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga  leo mjini Sumbawanga ambapo serikali imepongeza mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne ya mradi huo kupunguza udumavu.

Wadau wa toka wilaya wilaya tatu za mkoa wa Rukwa wakiwa kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu leo mjini Sumbawanga 

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Saleh Msanda akizunguza kwenye kikao cha wadau wa Lishe leo mjini Sumbawanga ambapo amezitaka halmashauri za Rukwa kutenga bajeti yenye uhalisia katika kutekeleza afua za lishe ili tatizo la udumavu kwenye jamii ilimazike.

Meneja wa Mradi wa USAID/ Lishe Endelevu Dkt. Benny Ngereza amesema mradi huo  umeweza kuwafikia walengwa wengi kwa kuwafundisha elimu ya ufugaji wa kuku bora na sungura pia kilimo cha bustani lengo la kuwezesha jamii kupata vyakula vyenye lishe bora.

Mkurugenzi wa mradi wa USAID/Lishe Endelevu Dkt. Joyceline Kaganda akizungumza na wadau wa lishe leo mjini Sumbawanga ambapo ameeleza kuwa katika miaka minne ya utekelezaji jumla ya vijiji 2000 katika mikoa ya Rukwa, Morogoro, Iringa na Dodoma imefikiwa ma kupatiwa elimu ya lishe bora.

Afisa Kilimo Mwandamizi toka Wizara ya Kilimo Bw. Makoye Thobias akizungumza lwenye kikao cha tathmini ya mradi wa Lishe Endelevu leo mjini Sumbawanga amesema wizara itaendelea kutoa miongozo ya uzalishaji mazao ya kilimo unaozingatia uopatikanaji wa lishe bora kwa jamii.

Bw. Japhet Msoga ambaye ni Mwakilishi wa Wizara ya Afya akizungumza kwenye kikao cha wadau wa lishe leo mjini Sumbawanga amesema suala la kupambana na udumavu linahita ushirikano wa pamoja na wadau na kuwa serikali imefanya suala hilo kuwa agenda ya kudumu .

Mwakilishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Bi. Josephine Manase ameshauri jamii ya wanaRukwa kuzingatia ulaji sahihi wa makundi ya chakula kutokana na uwepo wa vyakula vingi hatua itakayosaidia kuondoa tatizo la udumavu na utapiamlo.

Mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Wambura Messo ameitaka jamii iongeze kasi ya utumiaji vyakula vinavyokana na mazao ya mifugo kutokana na kuwa na viwango vikubwa vya lishe bora. Amesema hayo mjini Sumbawanga wakati wa kikao cha tathmini ya mradi wa Lishe Endelevu.

Mratibu wa Mradi wa Lishe Endelevu mkoa wa Rukwa Maria Machilu amesema jumla vya vituo 109 vya kutolea huduma za afya mkoani Rukwa vimefikiwa na kuwezesshwa kutoa elimu ya lishe bora kwa jamii.
Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

………………………………………..

Na. OMM Rukwa 

Serikali imelipongeza Shirika la USAID/Lishe Endelevu kwa kutekeleza mradi wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe bora hatua iliyosaidia mkoa wa Rukwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa mwaka 2021/2022 katika utekelezaji mikataba wa lishe kati ya mikoa 26.

Pongezi hizo zimetolewa leo (Novemba 24, 2022) mjini Sumbawanga na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba katika ufunguzi wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi huo unaotarajia kuisha mwaka 2023.

Akitaja mafanikio ya mradi huo, Waryuba alisema mradi wa Lishe Endelevu umesaidia halmashauri zote za Rukwa kwa sasa zinaweka bajeti katika afua za lishe na zinatoa pesa kutekeleza afua za lishe.

Mradi huo pia umetoa mafunzo kwa maafisa ugani ambao kwa kutumia stadi walizozifunza wameweza kuwajengea uwezo wakulima 13,416 jinsi ya kutumika mbinu bora za ufugaji na ukulima. 

Katika hatua nyingine Waryuba alitoa wito kwa Shirika hilo kufikiria kuendelea kubaki mkoani Rukwa ili kutokana na uhitaji wa elimu ya lishe bora kukabiliana na udumavu na kwenye jamii.

“Wito wetu kwenu wadau bado tunawahitaji mfikirie kuendelea kubaki mkoani Rukwa kutokana na uhitaji wetu katika kutekeleza masuala ya afua za lishe kwenye jamii “alisema Waryuba.

Kwa upande Mkurugenzi wa mradi wa USAD/Lishe Endelevu Dkt. Joyceline Kaganda alisema mradi umetekelezwa Rukwa kwa miaka minne tangu 2018 jamii imefanikiwa kuongeza ulaji wa vyakula vyenye protini kwa wingi ikiwemo samaki kupitia elimu ya ufugaji samaki kwenye mabwawa.. 

“Mradi unakwenda ukingoni lakini tunapigia debe wafadhili wasiondoke Rukwa na pia tunaomba serikali ichukue umiliki wa mradi huu baada ya Septemba 2023 ikiwemo kusimamia na kuwafuatilia maafisa ugani kutekeleza afua za lishe “alisema Dkt. Kaganda.

Kwa mujibu wa Dkt. Kaganda mradi wa Lishe Endelevu umefanikiwa pia kufikia vijiji zaidi ya 2000 katika mikoa minne iliyotekeleza mradi huo ambayo ni Rukwa, Morogoro, Dodoma na Iringa kwa kushirikiana na serikali kutekeleza afua za lishe.

Nao wawakilishi toka Wizara ya Kilimo Makoye Thobias na mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Wambura Messo walieleza kuwa serikali itaendelea kutoa miongozo kufanikisha agenda za lishe kwa ustawi wa wananchi.

Mradi wa Lishe Endelevu umelenga kuongeza juhudi za serikali katika kupambana na janga la udumavu kwa kuimarisha afya na lishe katika kundi la watoto wenye umri chini ya miaka mitano, vijana balehe na wakina mama walio katika umri wa kuzaa.

About the author

mzalendoeditor