Featured Kitaifa

DK.ISAKA ATAKA WATAFITI KUTOA MATOKEO YA TAFITI ZAO KWA JAMII

Written by mzalendoeditor

 

Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Irene Isaka ,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya  Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na  GIZ lililofanyika leo Novemba 24,2022 jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Profesa Emmanuel Luoga, akisoma risala wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mbuyuwayu AICC, lililofanyika leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Profesa Suzana Augustino ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika  leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Dkt. Irene Isaka ,akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa masuala ya Teknolojia na Tehama kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Ujerumani na GIZ mara baada ya Ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na GIZ lililofanyika  Leo Novemba 24,2022 Jijini Arusha.

……………………………….
Na Mwandishi wetu, Arusha

WATAFITI vijana wanaofanya tafiti katika nyanja mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameagizwa kutoa matokeo ya tafiti zao ili kutatua  changamoto zilizopo miongoni mwa jamii.

Hayo yamesemwa  leo Novemba 24, 2022 jijini Arusha na  Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Dkt. Irene Isaka ,wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la siku mbili la Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya  Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na  GIZ .

Amesema kuwa,   endapo watafiti vijana wakitoa matokeo ya tafiti zao kwa jamii serikali za nchi za Afrika Mashariki (EAC ) zinaweza  kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kukabiliana na  mabadiliko ya tabia nchi .

“Lazima sasa wasomi vijana wanapofanya tafiti zao wazitoe zisomwe ili serikali na jamii zichukue hatua katika kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa” amesema  Dkt. Irene 

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ,Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa CENIT@EA ni kituo cha Umahiri kinachojihusisha na masuala ya  Kompyuta na Tehama ambacho  kinahusisha nchi zote za Afrika Mashariki kwa lengo la kuhakikisha kuwa,  masuala ya tafiti yanaibuliwa ili kutoa majibu sahihi ya changamoto za jamii na kuibua ajira.

Aidha, Prof Luoga ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Ujerumani katika kuendeleza masuala ya elimu na tafiti kwa wanasayansi na wakufunzi kwa kipindi cha miaka saba tangu mwaka 2017.

Kwa upande wake  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki Profesa  Gaspard Banyankimbona  ameziomba serikali za nchi hizo kuweka fedha zaidi katika masuala ya tafiti,  kwa lengo la kutoa majibu sahihi ya changamoto katika sekta mbalimbali za kijamii,  ili kuwasaidia wasomi wanaofanya tafiti kutozifungia ndani bali wazitoe ili zisomwe na jamii ikiwemo idara mbalimbali na  kuchukua hatua thabiti.

About the author

mzalendoeditor