Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MANAYARA

Written by mzalendoeditor

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakati akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Catherine Magali aliyekuwa akielezea maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo Babati mkoani humo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali Wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo Babati katika ziara yake ya siku mbili Mkoani humo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa akisikiliza maelezo ya Ujenzi wa Ofisi za Chama hicho cha Mapinduzi, Babati Mkoani Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwasalimia Wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hizo za Chama Babati Mkoani Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hizo za Chama Babati Mkoani Manyara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Babati kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kwaraa Mkoani Manyara.

Wananchi pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Manyara wakiwa kwenye uwanja wa Kwaraa Babati kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 23 Novemba, 2022.

About the author

mzalendoeditor