Uncategorized

MBUNGE LUCY MAYENGA ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WANANCHI AMBAO NYUMBA ZAO ZIMESOMBWA NA MAJI SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (kushoto) akikabidhi chakula kwa mmoja wa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (katikati mwenye kiremba cheusi) akikabidhi chakula kwa mmoja wa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
 
Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (CCM) ametembelea na kuzipatia msaada wa chakula (mahindi kilo 900) kaya 10 za wananchi wa mtaa wa Ndembezi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji kufuatia mvua iliyonyesha.

Mhe. Mayenga amekabidhi msaada huo leo Novemba 22,2022 alipotembelea wakazi hao katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Ndembezi akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga.
 
Akikabidhi msaada huo, Mhe. Lucy Mayenga amesema kuwa ameguswa na tukio la wakazi 10 wanaoishi katika mtaa huo nyumba zao kuezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji na kuamua kuwatembelea kuwapa pole ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi kila kaya iliyoathiriki kilogramu 50 za mahindi ikiwa ni njia moja wapo itakayosaidia wakazi hao kuondokana na adha ya kukosa chakula katika kipindi hiki ambacho wanaangalia namna ya kuezeka nyumba zao.
 
“Natoa pole sana kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji. Nilipata taarifa ya ninyi kupatwa na changamoto hii nikiwa bungeni na ndiyo maana nimeamua kuja kuwapa pole na kutoa mahindi kidogo ambayo kila kaya inapata Kilo 50 ikiwa ni sehemu ya kuwapa pole ndugu zangu”, amesema Mayenga.
 
“Naomba niwaambie tuko pamoja sana katika kipindi hiki kigumu ambacho kaya hizi 10 zinahangaika kutafuta mahali pa kuishi kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Novemba 11 mwaka huu”,ameongeza Mhe. Mayenga.
 
Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi Khamis Fufuji amesema kuwa mvua kubwa iliyosababisha maafa hayo ilinyesha Novemba ,11,2022 na kuezua nyumba 10 za wakazi wa mtaa huo hali iliyopelekea kaya hizo kukosa makazi na kulazimika kuomba makazi ya muda kwa majirani kwanai nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula kusombwa na maji.
 
Kwa upande wao baadhi ya waathirika wa tukio hilo ambao kwa sasa wamehama makazi yao akiwemo David Matine Mgoroka wamemshukuru Mhe. Lucy Mayenga kwa kuwapa msaada wa mahindi kwani chakula hicho kitawasaidia katika kipindi hiki ambacho wameomba makazi ya umda kwa majirani na kuwaomba watu wengine walioguswa na tukio hilo kuangalia namna ya kuwasaidia kuezeka nyumba zao ili waweze kurudi katika makazi yao ya awali kwa wakati.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (katikati) akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Ndembezi baada ya kuwasili kuwapatia chakula wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
Muonekano wa sehemu ya mahindi yaliyotolewa na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (CCM) kwa wananchi wa mtaa wa Ndembezi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Ndembezi kabla ya kuwapatia chakula wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (katikati mwenye kiremba cheusi) akikabidhi chakula kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Mhe. Grace Samwel akizungumza wakati Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (kulia) akikabidhi chakula kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akizungumza wakati Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akikabidhi chakula kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi Khamis Fufuji akizungumza wakati Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akikabidhi chakula kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Kata ya Ndembezi Issa Stima akizungumza wakati Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akikabidhi chakula kwa wananchi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo na chakula chao kusombwa na maji.

About the author

mzalendoeditor