Na Bolgas Odilo_Mzalendo
MABINGWA Watetezi Yanga wamerejea kileleni Mwa Msimamo baada ya kuizamisha mabao 4_1 Singida Big Star Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kucheza mechi tano bila bao hatimaye Mshambuliaji hatari kunako Ligi Fiston Mayele amezinduka na kupiga Hat_Trick yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga akitokea AS Vita ya Congo na ikiwa ya Kwanza Msimu huu wa Ligi.
Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia pasi ya Jesus Moloko na katika dakika ya 26 Mayele alirudi tena kambani akimalizia pasi ya Fei Toto.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuiendelea kuishambulia Singida kunako dakika ya 48 Kibwana Shomary alipigilia msumari wa tatu akimalizia pasi ya Fiston Mayele.
Mayele alipiga hat_trick mnoo dakika ya 56 akimalizia pasi ya Joyce Lomalisa hata hivyo Singida walipata bao la kufutia machozi dakika ya 66 likifungwa na Medie Kagere.
Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 26 wakiwa wamecheza mechi 10 na kuishusha Azam FC yenye Pointi 26 wakiwa wamecheza mechi 12 na Simba wameshuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 24 wakicheza mechi 11.
Matokeo mengine Ihefu imepoteza mabao 2_1 dhidi ya Polisi Tanzania wakiwa nyumbani na Kagera Sugar wametoka sare ya kufungana mabao 2_2 na wenyeji Mbeya City