Featured Kitaifa

KIHONGOSI :CHAGUENI VIONGOZI BORA

Written by mzalendoeditor

 

KATIBU  wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi,akizungumza kwenye  Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Mkoa wa Dodoma,uliofanyika leo Novemba 16,2022 jijini Dodoma.

KATIBU wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Mkoa wa Dodoma,uliofanyika leo Novemba 16,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma anayemaliza muda wake, Billy Chidabwa,akiwashukuru vijana kwa kumwamini katika kipindi cha Miaka mitano wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Mkoa wa Dodoma,uliofanyika leo Novemba 16,2022 jijini Dodoma.

Sehemu ya wagombea wa nafasi mbalimbali katika nafasi za Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) 

………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU  wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi,amewataka vijana wanaowania nafasi kuwa wakakitumikie Chama na sio watu ndani ya CCM.

Hayo ameyasema leo Novemba 16,2022 jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, ambapo amewataka kuchagua viongozi bora wenye maadili .

Kihongosi, amewataka kuchagua viongozi ambao hawafanyi kazi kwa maslahi yao bali waende kukitumikia chama pamoja na kusimamia misingi ya CCM.

“Tunaochagua kiongozi tujue tunachagua mtu wa kutuongoza kwa miaka mitano, tukichagua vizuri tutakwenda vizuri mkichagua vibaya, maamuzi mnayo nyie, lakini viongozi watakaokwenda kusaidia pamoja na  kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, msituletee viongozi watakaokwenda kufanya kazi kwa maslahi yao.”amesema Kihongosi,

Aidha amesema kuwa mara baada ya uchaguzi ukiisha wanapaswa kuvunja makundi ili kukijenga chama na jumuiya kwa ujumla.

“Twendeni tukachague watu ambao watakaokuwa wanyenyekevu na si wanyenyekevu ndani ya watu ndani ya CCM, mkifanya hivyo mtakwenda kukitendea haki chama kumtendea haki Rais wetu na vijana wa nchi hii,”amesisitiza

Kwa upande wake  Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga  amewasisitiza watakaochaguliwa kutambua wajibu wao kwenye nafasi wanazozitumikia na si kwa ajili ya kupiga kura pekee.

Naye ,Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo anayemaliza muda wake, Billy Chidabwa, amewataka viongozi watakaochaguliwa kuwa na mshikamano na ushirikiano na vijana wenzao.

About the author

mzalendoeditor