Featured Kitaifa

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUFANYIKA LINDI

Written by mzalendoeditor
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya 
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi kuanzia Novemba 24 na kilele chake ni Disemba Mosi 2022 mwaka huu.
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene,akisisitiza jambo kwa na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya 
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi kuanzia Novemba 24 na kilele chake ni Disemba Mosi 2022 mwaka huu.
 
MKURUGENZI  Mtendaji,Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko,akizungumza  na wandishi wa habari kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Dunia Desemba Mosi mwaka huu.
MKURUGENZI Mkazi wa UNAIDS Tanzania, Martin Odiit,,akizungumza  kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Dunia Desemba Mosi mwaka huu.
 
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa taarifa kuhusu 
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi kuanzia Novemba 24 na kilele chake ni Disemba Mosi 2022 mwaka huu.
…………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
TUME  ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeeleza kuwa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yamepungua kutoka watu 110,000 mwaka 2016/17 hadi kufikia 54,000 mwaka 2020/2021.
Hayo yameelezwa leo Novemba 14,2022 na Mkurugenzi Mtendaji,Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, wakati akizungumzia na wandishi wa habari kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Dunia Desemba Mosi mwaka huu.
Dk Maboko amesema idadi ya vifo pia imepungua kutoka vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi 64,000 mwaka 2016/17 hadi kufikia vifo 29,000 mwaka 2020/21.
“Pamoja na mafanikio hayo lakini bado tunahitaji kuongeza nguvu ili kufikia malengo ya sifiri tatu ifikapo mwaka 2030,”amesema
Dk Maboko ametoa wito kwa jamii na wadau wote kushirikiana katika kupanga na kutekeleza shughuli za kuthibiti VVU na UKIMWI kwa kuzingatia vipaumbele.
Ameyataka maeneo ya vipaumbele ni kuimarisha afua za VVU na UKIMWI kwa vijana ambapo takwimu zinaonesha kuwa kundi la vijana wa umri wa miaka 15-24 linachangia maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 30.
“Hivyo kulifanya kundi hili kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya VVU.Kwa mukhtadha huo maadhimisho ya mwaka huu yanatoa vipaumbele pia kwa vijana kushiriki kikamilifu,”amesema Dk.Maboko.
Amesema matukio yatakayofanyika ni pamoja na maonesho ya shughuli za wadau wa kudhibiti VVU na UKIMWI yatakayoanza Novemba 24 mwaka huu hadi Disemba mosi mwaka huu katika uwanja wa Ilulu Lindi.
Dk.Maboko amesema kutakuwa na maonesho ya utoaji wa Huduma rafiki kwa vijana  kuanzia Novemba 24 Hadi 30.
Amesema vijana watatengewa eneo Maalum litakalojulikana kama Kijiji cha vijana  ndani ya uwanja wa Ilulu Lindi.
Vilevile,amesema kutakuwa na mdahalo wa viongozi wa dini pamoja na vijana unaotarajiwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Dk John Jingu.
“Kutakuwa na mdahalo wa vijana wa vyuo vikuu na kati vilivyopo mkoani Lindi kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na afua za VVU na UKIMWI.
“Mbio za marathon kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa mfuko wa udhamini wa kuthibiti UKIMWI,”amesema
Amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mawaziri,Mabalozi,wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na viongozi wa dini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene, amesema kuwa maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi kuanzia Novemba 24 na kilele chake ni Disemba mosi 2022 maadhimisho yatakayoambatana na shughuli mbalimbali kuhamasisha watu kutambua hali zao.

Simbachawene amesema maadhimisho hayo yamelenga kutoa fursa ya kuthathmini hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa virus vya ukimwi kitaifa na kimataifa.

 “Hapa nchini maadhimisho yatafanyika kitaifa mjini Lindi wadau wa kitaifa chini ya uratibu wa TACAIDS wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya kutoa huduma muhimu wakati wa maadhimisho hayo ikiwamo utoaji wa taarifa na habari muhimu za kudhibiti VVU na Ukimwi” amesema 

Ameongeza kuwa “Katika maadhimisho tunatumia kuhamasisha viongozi na jamii kuendelea kutoa kipaumbele kwa agenda ya kudhibitiVVU na Ukimwi na kujumuishwa katika mpango wa maendeleo ya nchi” amesema Waziri Simbachawene

Aidha Simbachawene  ameitaka amewataka mikoa yote nchini kuandaa na kuadhimisha siku hiyo yenye kaulimbiu ya “imarisha usawa”

About the author

mzalendoeditor