Featured Kitaifa

WADAU WAIOMBA SERIKALI KUSIMAMIA TOZO ZA MKAA.

Written by mzalendoeditor

Sehemu ya Magunia ya Mkaa na ujazi wake kwenye vijiji vinavyotekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu na Uvunaji endelevu wa Misitu.

Afisa Kujenga uwezo kutoka Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) Bwana Simon Lugazo wakati akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari(Hawapo Pichani) nje ya mkutano huo baada wa Wadau wa Kikosi kazi cha Misitu Tanzania.

Afisa Maliasili wa Mkoa wa Morogoro bwana Joseph Chuwa akieleza changamoto za uhifadhi wa Misitu na mapendekezo yake mbele ya Waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mara baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano huo wa Wadau wa Kikosi kazi cha Misitu Tanzania.

Picha ya Pamoja ya Wadau walioshiriki kwenye mkuatano wa Wadau wa  Kikosi kazi cha Misitu Tanzania (TFWG) Kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Waandishi wa Habari.

Sehemu ya Magunia ya Mkaa na ujazi wake kwenye vijiji vinavyotekeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu na Uvunaji endelevu wa Misitu.

Tanuli la kisasa la uchomaji wa Mkaa ambalo limeboreshwa na kutumiwa na wachoma mkaa kwenye vijiji vinavyoshiriki Mradi kupitia mashirika ya TFCG na MJUMITA ili kupata mkaa bora.

Wananchi wakivuna Mbao kwenye vijiji vinavyoshiriki mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu na uvunaji endelevu wa mazao ya Misitu.

……………………………………….

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Zaidi ya shilingi bilioni 460 zinapotea kwa mwaka kutokana na mapato yatokanayo na kodi pamoja na tozo mbalimbali za mauzo ya biashara ya Mkaa nchini kwenye tani 1,895,248 sawa na kilo bilioni 1.89 zilizoripotiwa kuzalishwa mwaka 2021.

Afisa Kujenga uwezo kutoka Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) Bwana Simon Lugazo ameyaeleza hayo wakati akiwakilisha mada kuhusu Ushahidi wa matokeo hasi ya kubadilika kwa kanuni ikiwemo GN417 kwenye mkutano wa wadau na wanachama wa Kikosi kazi cha Misitu Tanzania (TFWG) uliofanyika Mkoani Morogoro.

Alisema kwa mujibu wa ripoti ya Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2021 imebainisha kuwa thamani ya biashara ya Mkaa nchini ni shilingi 2,056,771,556,434 ambapo katika fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 9.9 ni tozo na kodi iliyokusanya na kuingia serikalini kutokana na mkaa unazalishwa nje ya vijiji vyenye usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii hizi ni zile zilizokamatwa na kupita kihalali lakini mkaa mwingi zaidi ya huo unapita kwa njia za magendo na unavunwa kwa njia zisizo halali ambao tunauona unapita na mapikipiki kuelekea mijini.

Aliongeza kusema kuwa awali kulikuwa na mafanikio makubwa katika uhifadhi Misitu ya Vijiji kupitia mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu Jamii kupitia uvunaji endelevu wa biashara ya Mkaaa na mbao na kuchangia jamii kuhifadhi na kulinda misitu na kupata fedha za kutelekeza miradi mbalimbali ya maendeleo  kwenye vijiji kutokana na mapato hayo lakini baada ya ujio wa GN417 uzalishaji na usimamizi umeshuka kwakuwa jamii haipati tena motisha.

Lugaza alisema awali kabla ya GN417 serikali za   vijiji yalijengewa uwezo na kupewa mamlaka ya kuanzisha na kufanya shuhuli za uvunaji kwenye misitu ya vijiji kwa njia endelevu na kupanga bei za kuuza mazao hayo ya misitu hususani mkaa na mbao kupitia sharia ya misitu ibara ya 49(6) kwa kutoa vibali vya uvunaji na kupanga bei.

“Mkaa endelevu kwenye vijiji 30 vya mkoa wa Morogoro ambavyo vinatekeleza mradi wa mkaa endelevu na usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji kati ya mwezi wa 12 mwaka 2015 hadi Septemba mwaka 2021 yameonesha kuwa yameanguka kwa baada ya ujio wa GN417 katikati mwa mwaka 2019 kwa shilingi bilioni 1.3 kwa kwa kipindi cha miezi 24.

Amefafanua kuwa hali hiyo inatokana na kwamba gunia moja la Mkaa kwa bei ya Serikali  linatakiwa kuuzwa kwa shilingi 42,648 ambayo ndio bei inayojumlisha kodi na tozo mbalimbali zilizo rasmi zaa serikali wakati mkaa unauzwa kwa shilingi elfu 30,420 kwenye maeneo ambayo hayana mfumo huo wa uhifadhi shirikishi wa misitu na uvunaji endelevu wa mkaa hali ambayo inawafanya wanunuzi kukimbilia kwenye maeneo hayo yanayovuna bila kuzingatia uendelevu wa misitu wala usimamizi.

Aidha  kwa mujibu wa utafiti walioufanya ulionesha kuwa mwaka 2018 kulikuwa na miradi 43 yenye thama ni za zaidi ya shilingi milioni 229 iliyokuwa inatekelezwa kutokana na biashara ya Mkaa kwenye vijiji 30 vya mradi Mkoani Morogoro lakini baada ya ujio wa GN417 miradi imeshuka hadi kufikia million 13 pekee.

Kwa upande wake Afisa Maliasili wa Mkoa wa Morogoro bwana Joseph Chuwa amesema GN417 ni ya Tanzania nzima sio vijiji vinavyotekeleza mradi pakee na ili kukomesha tatizo hilo ni muhimu sasa kuongeza nguvu katika kudhibiti maeneo ambayo yanachoma mkaa kwa njia holela ili mkaa uweze kutoka kwenye vijiji vyenye mpango wa usimamaizi shirikishi wa misitu na uvunaji endelevu.

Amesema Sera na Sharia za Misitu ni za Tanzania nzima hivyo ni vyema kukawa na mfumo mmoja wa usimamizi wa Misitu yote Tanzania kutoka Misitu ya Serikali mpaka ya mtu binafsi hii haina maana kuwa inaondoa haki ya umiliki wa mtu mmojammoja bali isaidie kudhibiti na kusimamia Misitu yote.

“Asilimia 48 hadi 50 ya Misitu yote ambayo ipo hatarini kutoweka ipo kwenye ardhi za vijiji na inapungua kila mwaka nadhani kuwe na ubia kwa maana ya Serikali kuu,TFS,Halmashauri na Vijiji vyenyewe kwenye kuisiamamia hii Misitu ya vijiji maana kwa mtazamo wangu naona kama uwezo wa vijiji kuisimamia unakuwa mdogo kwa maana ya vitendea kazi,fedha na utaalamu”alisema Chuwa.

Aliongeza “Hii izingatie pia kwenye kugawana keki itokanayo na Misitu hiyo kwa maana vijiji vyenyewe vipate mgao mkubwa, Halmashauri nazo zipate mgao na hivyohivyo kwa TFS na Serikali kuu kwahiyo kila mmoja ataona Misitu ina faida kwake na kuongeza nguvu kwenye uhifadhi wa misitu hiyo isivunwe kiholela kama ilivyo sasa”.

About the author

mzalendoeditor