Featured Kitaifa

KITUO KIKUBWA CHA UMAHIRI KUANZA KUJENGWA NA ERB

Written by mzalendoeditor

MSAJILI wa Bodi ya Usjali wa Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma wakati  akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa,akizungumzia na waandishi na habari (hawapo pichani) kuhusu mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita mara baada ya Msajili wa Bodi ya Usjali wa Wahandisi Nchini (ERB) Mhandisi Benard Kavishe ,kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023 leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma.

……………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

BODI ya usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) inatarajia kujenga kituo Kikubwa Cha Umahiri eneo la kizota, Jijini Dodoma ambapo ni Moja ya Vipaumbele vyake ili vijana waweze kufanya shughuli zao kwa kuonyesha ubunifu wao.

Hayo yameelezwa leo Novemba 10,2022 jijini Dodoma na Msajili wa Bodi hiyo,Mhandisi Bernard Kavishe ,wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya  Bodi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka 2022/2023 .

Mhandisi Kavishe amesema kutokana na kuwepo kwa Vijana wengi wenye mawazo ya kibunifu ila wanakosa namna ya kuendeleza mpaka kufika sokoni ,hivyo kituo hicho kitakuwa eneo sahihi la kuendeleza mawazo hayo.

“Kuna vijana wengi wenye mawazo mazuri kabisa ila namna ya kuendeleza inawawia vigumu sana ila tumeona sisi kama bodi suluhisho lake ni kujenga kituo cha umahiri ambapo itatumika kuendeleza vijana na Itakuwa na maabara pia,” Amesema Mhandisi Kavishe

Aidha Mhandisi Kavishe, amesema kuwa rushwa bado ni kikwazo kikubwa katika sekta hiyo nchini hali inayosababisha watu wasio na uwezo kupatiwa kazi katika maeneo mbalimbali.

“Rushwa bado ni kansa ya taifa katika maeneo mbalimbali kweli bado wapo watu ambao wanajihusisha na vitendo vya rushwa lakini sisi tunapo wabaini tunawafikisha katika vyombo vyenye mamlaka na suala hilo kama vile TAKUKURU na wengine”amesema Mhandisi  Kavishe

Vilevile, Mhandisi Kavishe amesema kikwazo kingine wanachokabiliana nacho ni vishoka walipo katika sekta hiyo hivi sasa.

“Vishoka ni ‘crime’ kama ambavyo ilivyo katika tasnia nyingine mtu kujifanya Daktari wakati siyo taaluma yake anastahili kushitakiwa na kufungwa kama mharifu mwingine”amesema

 Mhandisi Kavishe amesema kuwa ,kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya Wahandisi 33,773, kati yao 26,000 wapo katika soko la ajiri huku wenye leseni za Uhandisi wakiwa ni 10,000 na wengi wao wanashiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa inayoendelea.
“Tanzania tunakadiriwa kuwa na jumla ya Wahandisi 33,773 kati yao 26,000 wapo Sokoni na kati ya hao wenye leseni za Uhandisi wakiwa ni 10,0000 tu ,
Na kuongeza kuwa” Tuna Mafundi sanifu 1,979 na maabara za kihandisi 40 si mnajua mnapotaka kujenga ni lazima eneo lipimwa na iangaliwe pia kwa eneo unalotaka kujenga ni aina gani au ni muundo gani inayostahili kutoakana na mazingira kwa ujumla hapo ndio kazi ya maabara zetu zinaanzia,”Amesema Mhandisi Kavishe
Mhandisi Kavishe amesema kuwa Bodi hiyo imeshasajili Makampuni 398 inayojishuhulisha na masuala ya uhandisi huku makapuni 275 kati ya hayo ni ya ndani ya nchi wakati makampuni 123 yakiwa ni kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa, ameipongeza bodi hiyo kwa namna ambavyo imendelea kutekeleza majukumu yake ya kusimamia wahandisi wakati huu ambao taifa likiwa linatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.
“Nafasi ya ERB ni kubwa  katika maendeleo ya Taifa letu kwani kila penye Mradi unaoendelea ERB wapo na wanathibiti ubora wa kazi na wa Mhandisi anayejenga ule mradi hivyo niwaambieni tu hii ni bodi kongwe na haya majengo mnayoyaona yote kuna Mkono wa ERB,”Amesema Msigwa
Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Imeanzishwa Mwaka 1968, ikiwa na majukumu ya Kusajili Wahandisi,kuendeleza wahandisi na kutoa hithibati kwa waandisi , hayo majukumu yote ERB inayatekeleza kwa ajili ya usalama wa nchi na kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

About the author

mzalendoeditor