Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul Novemba 03, 2022 Uwanja wa Jamhuri Morogoro amekabidhi Kombe kwa Timu ya TAMISEMI QUEENS ambao wameibuka Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa ya Muungano mchezo wa Netiboli mwaka 2022, baada ya kuifunga timu ya Kikosi Cha Valentia Zanzibar ( KVZ ) kwa jumla ya magoli 56 kwa 40.
Mhe.Gekul, pia amegawa vyeti na zawadi kwa wanamichezo bora, timu zilizoshiriki pamoja na waamuzi wa ligi hiyo.
Aidha, ligi hiyo imepata timu ambazo zitashiriki Mashindano ya Afrika Mashariki mapema mwaka 2023 ambazo kwa Tanzania Bara ni TAMISEMI QUEENS, JKT Mbweni, Nyika Queens, Magereza Tanzania (Morogoro)
Nyingine ni kutoka Tanzania visiwani ambazo ni KVZ, Zimatoto, Mafunzo na JKU, huku wanaume wakiwakiliswa na Bandari Veterans na Smart Boys
Mashindano hayo yalianza Oktoba 25, 2022 ambapo timu nyingine zilizoshoriki ni Mafunzo, JKT, Magereza, Nyika, Zimamoto, Kampala University, huku wanaume wakishiriki kupitia timu ya JKU Zanzibar, Samart Boys pamoja na Bandari Veteran za Tanzania Bara.