Featured Kitaifa

WINGI WA WANAWAKE KATIKA MATOKEO YA SENSA KWAMWIBUA MWENYEKITI UWT

Written by mzalendoeditor

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa,Gaudentia Kabaka,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma kuhusu namna walivyopokea matokea ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi yaliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

……………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa,Gaudentia Kabaka,amewataka wanawake nchini kutumia matokea ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi yaliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kama fursa kwa kuonyesha ubora kiutendaji.

Hayo ameyasema leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyopokea matokeo hayo.

Bi.Kabaka amesema  kuwa idadi  imeonyesha wanawake wanazidi kupaa na hawataki kuwa chini hivyo hawapaswi kujibweteka na badala yake  wapambane katika kuleta maendeleo ya nchi kwa kumsaidia Rais Samia.

Amesema kuwa matokeo yanaonyesha kuwa watanzania tupo milioni 61.7 huku wanawake wakiwa wakiwa ni asilimia 51 na wanaume asilimia 49.

”UWT wana bahati ya kumpata Rais Samia ambaye kazi yake ina mahitaji makubwa na  wakati wote amekuwa akijitoa bila kujibakiza sababu ya upendo na huruma na ustahimilivu alionao kwa watanzania.”amesema Kabaka

Amesema hii inamaana kuwa  ongezeko la watu hivyo ni lazima huduma kama nishati, mawasiliano, maji, elimu, afya, usafiri viongezeke jambo ambalo Rais Samia alishaanza maandalizi .

Hivyo amewataka wanawake walipo makazini kutokata tamaa kwakuwa watafika mbali kimaendeleo ya nchi.

Aidha Kabaka ametoa wito kwa wazazi kutowanyanyapaa watoto wa kike kwenda shule maana ni jeshi kubwa la baadae na hiyo imeonekana kupitia matokeo ya sensa mwaka huu.

 ”Nazisihi sekta binafsi kuwatambua wanawake kuwa ni watu muhimu na wawapeleke kwenye mafunzo mbalimbali ili kuleta mchango kwenye taasisi zao.”amesisitiza

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa,Gaudentia Kabaka,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 1,2022 jijini Dodoma kuhusu namna walivyopokea matokea ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi yaliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Phillis Nyimbi,akitoa utambulisho kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa,Gaudentia Kabaka,(hayupo pichani) kuzungumza  na waandishi wa habari kuhusu namna walivyopokea matokea ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi yaliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

About the author

mzalendoeditor