Burudani Featured

VIPAJI VYA FILAMU VIHAMASISHWE MTAA KWA MTAA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu wa Bodi ya Filamu  Emmanuel Ndumukwa akieleza umuhimu wa Wadau wa Filamu kushiriki Tuzo za Filamu Msimu wa Pili 2022, Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Hivi karibuni.

………………………………..

Bodi ya Filamu imewataka Wadau wa Filamu kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa kuandaa mpango kazi mahususi wa kuhamasisha na kuibua Vipaji vipya vya Filamu na Michezo ya kuigizaji vinavyokuwepo katika ya ngazi mbalimbali hadi kufikia ngazi ya mitaa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu wa Bodi ya Filamu Emmanuel Ndumukwa wakati wa kikao cha Wadau wa Filamu ulioenda sambamba na ukusanyaji wa Filamu kwaajili ya Tuzo za Filamu Oktoba 29, 2022, Mkoani Shinyanga.

Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi huyo amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha Sanaa inazidi kukua na kuwanufaisha Wadau. Hivyo, Bodi inaendelea kuhamasisha dhamira hiyo iliyoanzishwa kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Ni rai yangu kwa Wadau kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa mikoa kuhakikisha Wadau wa Filamu waliopo maeneo yetu tunawatambua na kuwafikia ili fursa zinapojitokeza waweze kunufaika,” alisema Mkurugenzi

Wakati wa kikao hicho cha Wadau Bodi, ya Filamu imetumia fursa hiyo kuwahamasisha Wadau kupata huduma za Bodi Kidijitali katika maeneo mbalimbali. Hivyo, Wadau wanaweza pia kutumia Mfumo kupitia anuwani info.taffa katika kupakia Filamu za Tuzo za Filamu 2022 pamoja na uwasilishaji kutumia Maafisa Utamaduni wa mikoa.

Aidha, Mkurugenzi Ndumukwa amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo katika hatua za kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Sanaa tayari kiasi cha Shillingi  Billioni 1.5 kimeshatengwa kwaajili ya Wadau wa Sanaa ikiwemo Filamu ili kuboresha na kutengeneza kazi zao ambazo  zitapanua wigo wa masoko ndani na nje ya nchi kwa kuwanufaisha na kuwaongezea kipato.  

Afisa Utamadumi Mwandamizi Janeth Elias ameishukuru Bodi kwa kuchukua hatua ya kuwafikia Wadau mkoani Shinyanga kwani imewapa fursa ya kujadili fursa na changamoto mbalimbali za tasnia ya Filamu na kupata Elimu kuhusu namna bora ya kuongeza ubora wa Filamu kutoka Bodi.

Aidha, Bodi kufika na kukusanya Filamu mikoani ni hatua muhimu ambayo itasaidia ushiriki wa Wadau kwa urahisi na itaongeza wigo wa Wadau kushiriki.  

Kwa upande wake Neema Mushi Mwenyekiti Chama cha Waigizaji Mkoa wa Shinyanga ameshukuru Serikali kwa kuratibu Tuzo za Filamu Msimu wa Pili 2022 kwa kuwafikia Wadau mikoani kupitia Bodi ya Filamu.

 Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa Wadau wa Filamu kuchangamkia fursa ya kushiriki Tuzo za Filamu  ambayo itasaidia Wadau wa Filamu kupata fursa zaidi za kujiendeleza na kunufaika na Filamu. 

 

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu wa Bodi ya Filamu  Emmanuel Ndumukwa akieleza umuhimu wa Wadau wa Filamu kushiriki Tuzo za Filamu Msimu wa Pili 2022, Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Hivi karibuni

Afisa Utamaduni Mwandamizi Janeth Elias akifafanua jambo wakati wa Kikao na Wadau wa Filamu Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Gabriel Hoka akieleza namna Bodi ya Filamu inavyotoa huduma kwa Wadau kupitia Mifumo mbalimbali ya TEHAMA wakati wa Kikao na Wadau wa Filamu Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Afisa Filamu Irene Ngao akieleza majukumu ya Bodi ya Filamu wakati wa Kikao na Wadau wa Filamu Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

 Mdau wa Filamu Mwl. John Tungu pia Mjumbe wa Baraza la Chama cha Waigizaji Mkoa wa Shinyanga akitoa maoni na kueleza baadhi ya changamoto katika tasnia ya Filamu ili kuboresha na kuendeleza tasnia hiyo.

About the author

mzalendoeditor