Featured Kitaifa

RAIS SAMIA:”TANZANIA INA WATU MILIONI 61.7′

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika sherehe za hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa Serikali kuanza kutumia matokeo ya Sensa katika kupanga miradi na mipango jumuishi ya maendeleo endelevu kwa wananchi.

Rais Samia ametoa wito huo leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma wakati akizindua matokeo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 pamoja na Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 Rais Samia ametangaza kuwa Tanzania ina idadi ya watu Milioni 61,741,120 ambapo watu 59,851,347 wapo Tanzania Bara na watu 1,889,773 wapo Zanzibar. 

Rais Samia amesema katika idadi hiyo wanawake ni milioni 31.6 sawa na asilimia 51 wakati wanaume ni milioni 30.5 sawa na asilimia 49.

”Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini ambao ni milioni 5.3 sawa na asilimia 8.7 na kufuatiwa na Mwanza yenye watu milioni 3.6 sawa na asilimia 6.
Rais Samia amesema katika  kipindi cha miaka kumi iliyopita Tanzania ilikuwa na watu 44,928,923, hivyo kuna ongezeko la watu 16,812,197 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 kwa mwaka kati ya mwaka 2012 na mwaka 2022. 

Rais Samia amesema Serikali imeandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ili utumike katika kutunga na kutekeleza sera na mipango ya maendeleo ya kisekta katika ngazi zote za utawala.  

Kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo, na Sensa ya Anwani za Makazi ya mwaka 2022 kumeifanya Tanzania kuandika historia kwa kuwa takwimu hizo zitawezesha kufuatilia na kutathmini Sera za Mipango Miji na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi ili kuwapatia huduma za kijamii.

Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi  amesema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wanatambua umuhimu wa takwimu hizo katika kupanga mipango mbalimbali  na wako tayari kufanya maamuzi sahihi katika maendeleo.

“Bila shaka mwongozo wa Taifa wa matumizi wa sensa ya watu na makazi 2022, utaongeza wigo wa matumizi matokeo ya sensa katika kuandaa taarifa na mipango jumuishi katika maendeleo,”amesema Rais Dkt.Mwinyi

Amesema mwongozo huo unadhihirisha dhamira ya dhati na Serikali zote mbili katika kuhakikisha wanatumia vyema raslimali zilizopo na kufanya maamuuzi sahihi katika kupanga na kutekeleza mipango.

Amesema watawezaweza kupanga mipango na kutekeleza kwa kutumia ushahidi wa takwimu ili maamuzi hayo yawe yanaakisi kwa maana idadi ya watu na mazingira yao.

Naye Mwenyekiti wa Taifa ya Sensa, Kassim Majaliwa ,ameahidi kuwa watatumia  takwimu hizo katika kupanga Mipango ya maendeleo.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti mwenza wa Sensa,Hemed Suleiman Abdulah amesema kuwa Sensa hiyo itawasaidia katika masuala ya Kitaifa na Kimataifa na Wataalam kuzifqnyia uchambuzi takwimu hizo za sesnsa.

Naye Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, ametoa wito kwa taasisi na watanzania wote, kutumia takwimu ambazo zipo kwenye Ofisi ya Takwimu (NBS)
Awali  Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa amesema kupitia sensa ya anwani na makazi wamechukua takwimu zote za wafanyabiashara wadogo na mahali biashara zao zilipo.
“Itakuwa ni rahisi kwa sekta ya benki kutoa mikopo ya kutosha kwa akinamama ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza vipato vyao,”amesema Dk Chuwa.

Amesema kazi iliyobaki hivi ofisi yake kufanya uchambuzi wa kina kuhusu masuala ya elimu, shughuli za kikazi, makazi ya watu wanayoishi, mazingira yao na itashirikisha watu wote ili matokeo hayo yafanyiwe uchambuzi wa kina na kuingia katika sera za nchi.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,akizungumza na  Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma waliofika kushuhudia uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

MAKAMO wa Pili wa Rais,Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Hemed Suleiman Abdulla,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

Mtwakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa,akielezea jinsi zoezi hilo la Sensa lilivyofanyika kwa ufanisi mkubwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU  ya viongozi pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

Vikundi mbalimbali vya Ngoma za asili na kwaya vikitumbuiza katika sherehe za hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  Mwongozo wa Matumizi ya Takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika sherehe za hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika sherehe za hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika sherehe za hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Kitabu cha Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 mara baada ya kukizindua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Vitabu vya Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

NDEGE ikiwa juu imebeba matokeo ya Sensa mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,kuzindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor