Featured Michezo

TBA KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MICHEZO NZUGUNI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo-DODOMA

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) upo mbioni kujenga uwanja  wa kisasa wa soka   katika Nyumba 3500 za Viongozi Nzuguni Dodoma.

Hayo yameelezwa  na Mtendaji Mkuu wa TBA,Daudi Kondoro wakati akizungumza katika ziara ya wajumbe wa bodi ya Ushauri TBA ya  kutembelea miradi mbalimbali ambayo wanaitekeleza Jijini Dodoma.

Arch.Kondoro amesema kuwa kiwanja hicho kitakuwa na standard za kimataifa na kitatumiwa  na wafanyakazi wa wizara mbalimbali kufanya mazoezi na kucheza mechi.

Amesema kuwa pia watakuwa wakiukodisha kwa ajili ya mabonza pamoja na timu mbalimbali ikiwemo za ligi Kuu na daraja la kwanza  kuutumia  ili kuweza kujipatia kipato.

“Tumeishatenga eneo kwa ajili ya kazi hiyo tukimaliza ujenzi wa majengo ya Serikali tunahamia kwenye uwanja tunataka ule wenye standard za kutumika katika michuano mbalimbali,”alisema Arch.Kondoro

Kwa upande wao Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA)  wameridhishwa na miradi inayotekelezwa na TBA Dodoma huku ikihimiza kukamilika kwa wakati.

Akizungumza Mwenyekiti wa bodi hiyo,Dkt.Ombeni Swai amesema kuwa wajumbe wa bodi ya ushauri wa TBA wameridhishwa na wanaipongeza TBA kwa kutekeleza kwa ufanisi miradi hiyo.

Miradi waliyotembelea ni pamoja na ule  wa  Wakala wa Misitu (TFS) jengo la Kanda,jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),ujenzi wa nyumba 20 za viongozi wa Serikali na ujenzi wa jengo la ofisi ya Rais Utumishi Mtumba.

“Tumeona jinsi ambavyo miradi hii inasubiri hatua za mwisho wahusika kuhamia tumeona ubora wa kazi na tumeona ushirikiano wa timu kuanzia kwa Mkurugenzi Mkuu wa watu wengine.

“Tumeona timu ya wataalalmu, tumeona kazi nzuri na tunaimani sehemu zilizobakia zitakamilika kwa wakati,”amesema Dkt. Swai

Mtendaji Mkuu wa TBA,Arch.Daud Kondoro,akitoa maelezo kwa  wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) wakati wakikagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mtumba unaotekelezwa na TBA Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhandisi Amon Nghambi akitoa maelezo kwa  Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) baada ya kukagua Mradi wa ujenzi huo  unaotekelezwa na TBA uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch Dkt.Ombeni Swai,akitoa ushauri kwa Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhandisi Amon Nghambi mara baada ya  Wajumbe wa Bodi hiyo kutembelea mradi huo unaotekelezwa na TBA uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch Dkt.Ombeni Swai,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

 

MENEJA Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Victor Balthazar,akiwaeleza waandishi wa habari miradi wanayoisimamia  mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora lililopo Mtumba Mhandisi Amon Nghambi,akizungumzia hatua ya ujenzi huo ulipofikia wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri TBA kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA  jijini Dodoma.

 

Mradi wa Ujenzi wa  Jengo la OR.Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora lililopo Mtumba ukiendelea unaotekelezwa na TBA

 

WAJUMBE wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) wakimsikiliza Msimamizi wa uhandisi Mradi wa Nyumba 20 za Viongozi Nyumba 300 zilizopo Kisasa Mhandisi Immabaraka Shedafa wakati wa ziara ya bodi ya ushauri TBA kukagua miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

  

MUONEKANO wa Mradi wa Nyumba 20 za Viongozi Nyumba 300 zilizopo Kisasa jijini Dodoma.

 

WAJUMBE  wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA)wakipata maelezo ya Mchoro kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3500 zilizopo Nzuguni Bw.Fedrick Jackson mara baada ya wajumbe wa bodi ya ushauri wa TBA kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

 

MTENDAJI Mkuu wa TBA,Arch.Daud Kondoro,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Majengo (TBA) kutembelea Miradi Mitano inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

 

MUONEKANO wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 3500  za Viongozi zilizopo Nzuguni unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

MUONEKANO wa Mradi wa Jengo la Kanda la Wakala wa Misitu (TFS) unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

 

Meneja Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Victor Balthazar,akitoa maelezo kwa Bodi ya Ushauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unaotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

 

MUONEKANO wa Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor