Featured Michezo

YANGA YAICHAPA KMC LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo,MZALENDO BLOG

YANGA imeendelea kutunza rekodi yake ya kucheza bila kufungwa baada ya kufikisha mechi 44 bila kupoteza baada ya kuizamisha bao 1-0 KMC mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Shujaa wa Yanga ni Kiungo Mshambuliaji Fei Toto aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 80 baada ya kuachia shuti kali ndani ya 18 na kumuacha mlinda mlango wa KMC.

Kwa Ushindi huo Yanga wamerudi kileleni wakifikisha Pointi 17 na kuishusha Mtibwa Sugar yenye pointi 15 huku Simba akishika nafasi ya tatu akiwa na Pointi 13 akiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mchezo mwingi umepigwa katika uwanja wa Uhuru wenyeji Ruvu Shooting wamepoteza kwa kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold FC kutoka Geita.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo wa Mzizima Derby matajiri wa Chamazi Azam FC watawakaribisha wekundu wa Msimbazi Simba katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku

About the author

mzalendoeditor